Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

RAIS DKT. SAMIA ATOA ZAWADI YA KRISMASI KWA WATOTO YATIMA KITUO CHA HOPE MANISPAA YA KAHAMA


Mkuu wa wilaya ya Kahama , Festo Kiswaga kwa niaba ya mkuu wa mkoa wa Shinyanga Sophia Mjema , akikabidhi chakula mchele , maharage , mafuta ya kula na viungo mbalimbli kwa sikukuu ya Chrismasi kilichotolewa na Rais .Dkt.Samia Suluhu Hassan kwa watoto wanalelewa na kituo cha yatima cha New Hope Orphanage Centre kilichopo Mwime ya Ilindi Manispaa ya Kahama. Picha na Patrick Mabula.
Mkuu wa wilaya ya Kahama , Festo Kiswaga kwa niaba ya mkuu wa mkoa wa Shinyanga Dkt. Sophia Mjema , akiongea wakati wa kukabidhi chakula cha sikukuu ya Chrismasi kilichotolewa na Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan.
Mkuu wa idara ya Ustawi wa Jamii wa Manispaa ya Kahama , Robart Kwela akiongea wakati wa kukabidhi chakula na mbunzi mbili kwa kituo cha kulea yatima cha New Hope Orphanage Centre kilichopo mtaa wa Mwime Ilindi , Manispaa ya Kahama kilichotolewa na Rais Dkt Samia Suluhu Hassan kwa ajili ya sikukuu ya Krismasi.
Viongozi mbalimbali wa Chama na Serikali waliofika kwenye kukabidhi chakula cha sikukuu ya Krismas kilichotolewa kwa kituo cha kulea yatima cha New Hope Orphanage Centre kilichopo Mwime Ilindi , Manispaa ya Kahama .

Na Patrick Mabula , Kahama.

Watoto wanaolelewa katika kituo cha kulea yatima na wenye mazingira magumu cha New Hope Orphanage Centre kilichopo mtaa wa Mwime ya Ilindi kata ya Zongomela manispaa ya Kahama wamemshukuru Rais Dkt .Samia Suluhu Hassan kwa kuwapatia zawadi ya vyakula kwa ajili ya kusherekea Krismasi.

Watoto hao wametoa shukrani hiyo leo Ijumaa Desemba 23,2022 baada ya kupokea chakula hicho kilichotolewa kwa ajili ya kusherekea sikukuu ya Krismasi na kumshukuru Rais Samia kwa moyo wake wa upendo na kuwajali waweze kusherkea sikukuu ya Krismasi kama watoto wengine.


Akikabidhi chakula hicho mkuu wa wilaya ya Kahama, Mhe.  Festo Kiswaga kwa niaba ya mkuu wa mkoa wa Shinyanga , Sophia Mjema amesema Rais Dkt .Samia amekuwa akiguswa na watoto wanaolelewa katika vituo vya kulea yatima na wanaoishi kwenye mazingira magumu na amewapatia chakula hicho waweze kusherekea sikukuu ya Krismasi kama wenzao kwenye familia.


Kiswaga amesema anamshukuru Rais Dkt. Samia kwa kuwajali watoto wanaolelewa katika vituo vya yatima waweze kusherehekea sikukuu ya Krismasi kama watoto wengine katika familia na serikali itaendelea kuratibu malezi ya watoto miongoni mwa jamii kuhakikisha wanalindwa na kuwa salama na waweze kukua kwa misingi ya raia wema.

Awali katika maelezo yake mkuu wa idara ya ustawi wa jamii wa Manispaa ya Kahama , Robert Kwela amesema Rais Dkt.Samia amewiwa kutoa chakula hicho kwa watoto wa kituo cha kulea yatima cha Matumaini Mapya yaani(New Hope Orphanage Center washelekee sikukuu ya Krismasi kama wenzao waliopo miongoni mwa familia na amemshukuru kwa moyo huo wa kuwajali watoto hao.


Naye Kaimu afisa Ustawi wa Jamii wa Manispaa ya Kahama , Swaiba Chemchem akisoma taarifa ya kituo hicho kwa niaba ya mkurugenzi amesema kituo hicho kimekuwa msaada mkubwa kwa serikali katika kulea  watoto yatima na wanaotoka mazingira hatarishi jumla wapo 42 , wasichana ni 24 na wavulana 18 kati ya hao raia wa kigeni wawili kike mmoja na kiume mmoja.

Chemchem amesema vyakula alivyotoa Rais Dkt. Samia ni kilo 60 za mchele , mbuzi wawili , mafuta ya kula , maharage na viungo mbalimbali vya mboga ambapo umetolewa wito kwa wadau wengine na raia wema kujitoa kuwasaidia watoto wanaolelewa katika vituo yatima na Mungu atawabariki.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com