Msimamizi wa uchaguzi wa CCM, Dk Ali Mohamed Shein ambaye ni Rais mstaafu wa Zanzibar amemtangaza, Dk. Samia Suluhu Hassan kuwa Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi kwa mara nyingine baada ya kupigiwa kura za ndio 1914 kati 1915, Abdulrahman Kinana kuwa Makamu mwenyekiti wa CCM Bara baada ya kutetea nafasi hiyo baada ya kupigiwa kura za ndio 1913 kati ya 1915 huku Rais wa Zanzibar, Dk Hussein Mwinyi akichaguliwa kuwa Makamu Mwenyekiti wa Zanzibar,baada ya kupigiwa kura za ndio 1912.
Wakati huo huo idadi kubwa ya nafasi za wajumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM (NEC) zimechukuliwa na mawaziri ambapowalioshinda ni pamoja na Angelah Kairuki ambaye ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais (Tamisemi), Dk Ashatu Kijaji (Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwezekezaji), Angelina Mabula (Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi).
Mkutano wa kumi wa CCM umefanyika na haya ndio majina ya wajumbe waliochaguliwa kuwa wajumbe wa NEC-CCM kwa Tanzania bara.
WANAWAKE
1. Dkt Angelina S Mabula Kura 770
2. Dkt Ashatu Kijaji Kura 764
3. Christina Solomon Mndeme Kura 761
4. Hellen Makungu Kura 755
5. Fenela A. Mukangara Kura 747
6. Angellah J. Kairuki Kura``` 730
WANAUME
1. Mahenda Leonard 845
2. Bashungwa Innocent 720
3. Wasira Steven 680
4. Msome Jackson William 591
5. Kasheku Msukuma 587
6. Kasesela Richard 574
7. Wambura Chacha Mwita 545
8. Bashe Hussein 510
9. Nnauye Nape Mosses 508
10. Gwajima Josephat 497
11. January Makamba 452
12. Mwigulu Nchemba 450
13. Macha 435
14. Msengi Ibrahimu 428`
Social Plugin