Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

WAHUNI WAVUNJA MOCHWARI NA KUIBA MAITI


Mhudumu wa mochwari katika Kaunti ya Nayandarua nchini Kenya amesalia kinywa wazi, mapema Alhamisi asubuhi baada ya watu wasiojulikana kuvunja makafani hiyo na kuiba mwili wa marehemu.

Joseph Mbuthia Githundi, ambaye anafanya kazi kwenye mochwari ya Hospitali ya JM, alipigwa na butwaa baada ya kupata kwamba watu wasiojulikana walivamia mahali hapo usiku wa Jumatano.

Kwa mujibu wa ripoti ya Nation Africa, maiti iliyotoweka kwenye friji ilikuwa ya mvulana wa miaka 10, na polisi hatimaye waliweza kuipata kwenye 'septic tank' iliyoko karibu na mochwari hiyo baada ya kuitafuta.

Mwili huo ulipatikana salama na kurejeshwa kwenye mochwari, huku uchunguzi wa tukio hilo ukianza.

Ripoti zimebaini kwamba wafanyakazi wa vibarua waliokuwa wakiandamana kupinga kufutwa kazi na serikali ya kaunti huenda walihusika na tukio hilo, ila polisi wameahidi kufanya uchunguzi wa kina.


Kwa upande wake, Naibu kiongozi wa wengi wa Bunge la Nyandarua Mwangi Kagwe, alisema kuwa hospitali hiyo haitachukua miili yoyote hadi pale usalama utakapoimarishwa.

“Tumefanya mazungumzo na maafisa wa idara ya afya na tumekubaliana kwa mambo kadhaa ikiwemo, usalama kuimarishwa na ukuta kujengwa kwenye mochari hiyo,” MCA huyo aliongeza kusema.

Via Tuko News

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com