Mji wa Umuaja katika jimbo la Delta, Ethiopia ambako maji yanayoitwa 'River Ethiope' hutiririka, ni mahali ambapo watu wengi hupendelea kutembelea na kupiga picha.
Watu wanataka nini katika nchi hii?
Ni mto 'River Ethiope' ambao huwavutia wengi hapa.
Ardhi ambayo maji haya hutiririka ni mahali patakatifu kwani inasemekana ni maji yanayowapa watu nguvu, yanaponya magonjwa, yanawapa watu mambo mema, na yanawapa wale wanaotaka watoto na wanaotaka wake na mambo mengine.
Oyolu Lucky, mwanamke ambaye amekuwa akitunza maji ya mto huo kwa miaka 20, aliambia BBC Igbo jinsi baba yake alivyomweleza kuhusu chanzo cha maji hayo.
Kwa mujibu wa baba yake mwanasayansi wa kale ndiye aligundua maji haya ya mto kuwa na uwezo huo katika nyakati za kale kwa kuwa ni maji safi sana kuliko maji mengine.
Ilidaiwa mwindaji na kundi lake waliukata mti kisha kesho yake walipofika pale walikuta mti umesimama tena.
Watu waliokuwa pale walisema kuwa mti ule na maji yaliyotoka ndani yake ni baraka kwa wananchi wa kijiji hicho na kuwaambia waamini kuwa hiyo ni heshima ya pekee.
Alisema kuwa ni maji ambayo yalitoka chini ya mti mkubwa ambao umekua kwa miaka mingi, ambapo nguvu ya maji haya inasemekana kutoka hapo. Ni maji yanayotiririka hadi miji mingine mingi nchini humo na kuelekea usawa wa bahari ya 'Atlantic'.
Pia alisema mahujaji wengi hufika hapo ili kupata nguvu na kusali sala maalum inayojumuisha pia mapadri wengi.
Hakuna aliyethibitisha kisayansi, lakini wenyeji wa huko wamekuwa wakitumia maji hayo kwa miaka mingi kwa imani.
Na wanaoshuhudia wanasema unapofika kwenye mto huo na kusema unayotaka kwa mfano, umetafuta sana mtoto na kukosa.... ukiyapaka ama kuyaoga, na kuomba.... haitakuchukua muda kupata ulichotaka.
Na hicho ndicho kinachowafanya waamini kwamba mto huo ni zawadi kwa mungu na unatoa zawadi kwa watu.
Chanzo - BBC Swahili
Social Plugin