Inaaminika kuwa mbwa alisababisha moto katika nyumba usiku wa mkesha wa Krismasi baada ya kuwasha mashine ya kukaushia nywele (hairdryer) kwa bahati mbaya.
Mamlaka za huduma za Zimamoto Essex ilisema wafanyakazi walipigiwa simu ya dharura kuhusu nyumba iliyozingirwa na Moshi kutoka Hockley, Essex.
Zima moto walifanya kazi haraka kuzima moto huo kutokea chumbani.Mbwa huyo alikuwa akingoja kwenye mlango wa mbele wakati mwenye nyumba aliporudi na wote wawili walitibiwa kwa kuvuta moshi, Mamlaka ilisema.
Meneja Gary Shinn alisema: "Mmiliki wa nyumba alikuwa nje na akarudi na kukuta nyumba yake imejaa moshi.
“Tunaamini kuwa moto huo ulianza kwa sababu mashine ya kukaushia nywele iliyoachwa ikiwa imechomekwa na kwenye kitanda."Tunafikiri huenda mbwa aliruka juu ya kitanda na kuiwasha kwa bahati mbaya, na hatimaye kusababisha kuwaka moto kwenye kitanda na godoro."
Pindi tu unapomaliza kutumia vifaa vyovyote vya umeme kama vile vikaushio vya nywele na vya kunyoosha nywele tafadhali chukua muda kuvichomoa."
Chanzo - BBC SWAHILI
Social Plugin