Shirika lisilo la la kiserikali la GCI kwa kushirikiana na wadau wengine (TAI,WAYDS , Right to Life, TVMC), kupitia mradi wa acha UKATILI limetoa Elimu kwa jamii za Kata za Lyamidati, Nsalala na Itwangi juu ya KUTOKOMEZA vitendo vya UKATILI DHIDI ya wanawake na watoto ambapo zaidi ya watu 600 wamefikiwa (450 wa kike, 150 wa kiume) katika Kata hizo. Shirika hili linatekeleza mradi wa acha UKATILI ambapo mradi huu umejikita kahamasisha jamii kuachana na Mila na desturi kandamizi zinazochagiza vitendo vya UKATILI DHIDI ya wanawake na watoto.
Kwa kipindi chote cha siku 16 za kupinga ukatili, GCI imeendesha makongamano katika jamii kwa ufadhili WFT -TRUST ambapo kwa upande wa Kata ya Lyamidati GCI kwa kushirikiana na ofisi ya Mkurugenzi wa Halmashauri ya Shinyanga kupitia Idara ya Maendeleo ya jamii imehuisha mabaraza ya watoto kuanzia ngazi ya Kijiji hadi Kata pamoja na kuweka madawati kwa shule zote za Msingi na sekondari katika Kata ya Lyamidati, lengo likiwa ni kuimarisha mifumo ya KUTOKOMEZA vitendo vya UKATILI DHIDI ya wanawake na watoto, kuleta chachu ya uwazi na kupaza SAUTI kwa kutoa taarifa za vitendo vyote vya UKATILI katika mamlaka husika.
Miongoni mwa mashirika yaliyounganisha Nguvu kwa GCI ni TAI, WAOC, RIGHT TO LIFE na TVMC.