Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

MWILI WA ASKOFU ALIYEDAIWA KUPOTEA WAOKOTWA ZIWA VICTORIA




Jeshi la polisi mkoa wa Mwanza limethibitisha kupatikana kwa mwili wa askofu mstaafu wa kanisa la Angilikana Diocese ya Victoria Nyanza Boniface William, anayedaiwa kupotea tangu Novemba 28/2022 na mwili wake kukutwa ukielea ndani ya maji kando ya ziwa Victoria.

Kamanda ya Polisi mkoa wa Mwanza Wilbroad Mutafungwa amesema Askofu huyo aliaga familia yake na kuelekea wilayani Sengerema kwa ajili ya kupokea malipo ya mwisho ya shilingi milioni 2 na laki 5 baada ya kuuza eneo lake pamoja na nyumba kwa kanisa la KKKT Sengerema na hata hivyo hakuweza kulipwa fedha hizo na wanunuzi walimtaka aende na nyaraka za umiliki baada ya hapo hakurudi nyumbani

Kamanda Mutafungwa amesema uchunguzi wa tukio hilobado unaendelea.

Chanzo - EATV

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com