Mkurugenzi wa Jamiiforums Maxence Melo akiwa pamoja na Mkurugenzi mtendaji wa Umoja wa klabu za waandishi wa habari Tanzania (UTPC), Kenneth Simbaya wakisaini mkataba wa ushirikiano baina ya taasisi hizo mbili, hafla hiyo imefanyika katika ofisi za Jamiiforums leo Desemba 15,2022 Jijini Dar es SalaamMkurugenzi wa Jamiiforums Maxence Melo akiwa pamoja na Mkurugenzi mtendaji wa Umoja wa klabu za waandishi wa habari Tanzania (UTPC), Kenneth Simbaya wakipeana pongezi baada ya kuingia mkataba wa ushirikiano baina ya taasisi hizo mbili, hafla hiyo imefanyika katika ofisi za Jamiiforums leo Desemba 15,2022 Jijini Dar es Salaam Mkurugenzi wa Jamiiforums Maxence Melo akizungumza na waandishi wa habari katika hafla ya kuingia katika mashirikiano kati ya Umoja wa klabu za waandishi wa habari Tanzania (UTPC), na Asasi ya kiraia ya Jamii forums, hafla hiyo imefanyika leo Desemba 15,2022 Jijini Dar es Salaam. Mkurugenzi mtendaji wa Umoja wa klabu za waandishi wa habari Tanzania (UTPC), Kenneth Simbaya akizungumza na waandishi wa habari katika hafla ya kuingia katika mashirikiano kati ya Umoja wa klabu za waandishi wa habari Tanzania (UTPC), na Asasi ya kiraia ya Jamii forums, hafla hiyo imefanyika leo Desemba 15,2022 Jijini Dar es Salaam.
*******************
Na Emmanuel Mbatilo na Neema Victor Dar es salaam
Waandishi wa habari nchini, wametakiwa kuandika habari zinazoleta suluhu katika kuisaidia sarikali kupata majibu ya matatizo yanayoikumba jamii, ikiwemo kero za wananchi katika afya, Tabia nchi, Familia, na hata zinazoibua ufisadi.
Akizungumza leo Desemba 15,2022 Jijini Dar es Salaam, wakati wa kuingia katika mashirikiano kati ya Umoja wa klabu za waandishi wa habari Tanzania (UTPC), na Asasi ya kiraia ya Jamii forums Mkurugenzi wa Jamiiforums Maxence Melo, amesema kuwa jamii na serikali wanahitaji habari za kiuchunguzi ili kuweza kupata majibu ya kero zinazowakabili wananchi.
Amesema kuwa, waandishi wa habari wamekuwa wa dhana potovu ya kuhisi habari za uchunguzi ni kama ujasusi hivyo, kunahaja wanahabari kuwajengea uelewa juu ya habari za kiuchunguzi.
Aidha amesema kuwa, ushirikiano walioingia na UTPC una lengo la kuwajengea uwezo waandishi wa habari nchini, katika kuandaa habari za kiuchunguzi zenye maslahi kwa umma ili kuchochea uwajibikaji na utawala bora
Hata hivyo amesema kuwa waadishi wa habari watajengewa uwezo uwezo kuhusu usalama wa kidijitali, matumizi sahihi na bora ya vifaa na mifumo ya kidijitali na namna bora ya kutumia uwanja wa kidigitali kuendeleza kazi zao .
Kwa upande wake, Mkurugenzi mtendaji wa Umoja wa klabu za waandishi wa habari Tanzania (UTPC), Kenneth Simbaya amesema kuwa Mashirikiano hayo kati yao na Jamiiforum yatakuwa chachu ya kukuza tasnia ya habari na kuzalisha wanahabari wenye uwezo mkubwa, wa kufanya kazi katika dunia ya leo ya kidigitali na kuongeza maudhui yenye tija na uhakika mtandao.
Pia amesema yatasaidia watanzania kunufaika na taarifa zenye tija na zinazochochea uwajibikaji nchini.
Ushirikiano kati ya UTPC na Jamii forums utarahisisha kazi ya uhakiki wa taarifa kutoka sehemu mbalimbali nchini kwa kutumia klabu wanachama wa UTPC.
Ikumbukwe kuwa Mnamo Novemba 18,2022 Jamii forum ilizindua jukwaa la JamiiCheck ambalo ni jukwaa shirikishi la kuhakiki taarifa mbalimbali zinazosambaa mtandaoni na nje ya mtandao