MWENYEKITI wa Chama Cha Mapinduzi(CCM) Wilaya ya Bukoba Mjini mkoani Kagera Joas Muganyizi Zachwa ameamua kuvunja ukimya baada ya kuwepo kwa clip ya sauti ambayo ni ya kutengeneza inayomhusu yeye akihusishwa kuwatukana madiwani na Katibu wake wa zamani wa Chama.
Akizungumza kuhusu sauti hiyo Zachwa amesema ameona clip ya audio ( sauti) ikihusishwa na yeye akiwatukana madiwani na katibu wake wa zamani wa Chama ambapo amefafanua kwamba Clip hiyo ni ya kutengenezwa na ameanza kuchukua hatua za kisheria na kutaarifu vyombo vinavyohusika kushughulikia.
"Najua hii inafanyika kutokana na mimi kusimamia maelekezo ya Ilani ya CCM na misingi ya Chama chetu ya kushughulikia kero za wananchi hasa wafanyabiashara.
"Nataka niwahidi wanaCCM wa Wilaya ya Bukoba Mjini, CCM na Serikali yake itabaki kuwa salama na hatutasita kuwasemea wananchi kwani ndio maelekezo ya Ilani na viongozi wakuu wa Chama. Mungu ibariki CCM, Mungu ibariki Tanzania."
Social Plugin