*******************
NA EMMANUEL MBATILO
KLABU ya Simba imelazimika kugawana pointi moja na timu ya Kagera Sugar baada ya kutoka sare ya 1-1 kwenye mchezo huo ambao ulipigwa kwenye dimba la Kaitaba mkoani Kagera.
Kagera Sugar ilianza kupata bao kupitia kwa nyota wao Deus Bukenya dakika ya 15 kabla ya Henock Inonga ajasawazisha dakika ya 38 yaa mchezo na kuwapeleka mapumziko ubao ukisoma 1-1.
Simba Sc sasa wataendelea kuwa katika nafasi ya pili akiwa na pointi 38, wakati mahasimu wao Yanga wakiwa juu nafasi ya kwanza na pointi 44 huku Azam akishika nafasi ya tatu akiwa na pointi 37 baada ya kulazimishwa sare 1-1 na Geita Gold .
Social Plugin