*******************
NA EMMANUEL MBATILO
KLABU ya Simba Sc imefanikiwa kuondoka na alama tatu mbele ya timu ya KMC Fc kwa kuishushia kipigo cha mabao 3-1, mchezo ambao ulipigwa kwenye dimba la CCM Kirumba Jijini Mwanza.
Simba sc ilianza kupata bao kipindi cha kwanza kupitia kwa nahodha wao, John Bocco na kuwatanguliza mbele mpaka mapumziko wakiwa mbele kwa 1-0 kabla ya KMC kusawazisha.
Simba Sc ilipata bao la pili kupitia kwa nyota wao Okra na baadae bekiwao kisiki raia wa DR Congo, Henock Inonga akifunga mahesabu kwenye mchezo huo na kufanya matokeo kuwa 3-1.
Social Plugin