Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

SIMBA SC YAJICHIMBIA KILELENI, YAICHAPA COASTAL UNION 3-0


NA EMMANUEL MBATILO

KLABU ya Simba imefanikiwa kuondoka na alama tatu mbele ya Costal Union Fc baada ya kuitandika mabao 3-0 mchezo ambao ulipigwa kwenye dimba la Mkwakwani mkoani Tanga.

Simba Sc ililazimishwa sare katika kipindi cha kwanza licha ya kukosa nafasi nyingi za wazi huku Coastal Union wakionekana kujidhatiti kuzuia nafasi nyingi ambazo Simba wamekuwa wakizipata.

Moses Phiri leo ameonesha uhaiakisaidiana na Clautos Chama ambaye alilikamata dimba ipasavyo hasa kipindi cha pili na kufanya Moses Phiri kupachika bao zuri ambalo liliwafanya kuwa mbele.

Moses Phiri akuishia hapo baada ya mchezaji Shomari Kapombe kuchezewa rafu ndani ya kumi na nane iliwekwa mkwaju wa penati ambayo ilienda kupigwa na Phiri na kuweza kufikisha mabao 10 ndani ya ligi akimfikia mshambuliaji wa Yanga Fiston Kalala Mayele ambaye kesho anaingia uwanjani dhidi ya Tanzania Prison.

Simba Sc imepata bao la tatu kupitia kwa Chama na kufanya ubao usomeke 3-0.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com