Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

WADAU WAKUTANA KUJADILI CHANGAMOTO ZA HAKI ZA BINADAMU, UTAWALA BORA, MAADILI NA MAPAMBANO DHIDI YA RUSHWA


Na. Beatrice Sanga- MAELEZO

Katika kuelekea maadhimisho ya siku ya Haki za binadamu na Maadili Nchini wadau mbalimbali wakiwamo Tume ya Haki za Binadamu(THBUB), Sekretarieti ya maadili ya viongozi wa umma, Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU), na Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC) wamekutana katika ukumbi wa Karimjee Jijini Dar es Salaam kujadili changamoto za haki za binadamu, Utawala bora, Maadili na mapambano dhidi ya rushwa nchini ili kuleta uboreshwaji wa haki hizo.

Akizungumza katika kongamano Hilo Mkuu wa Wilaya ya Ilala Bw. Ng'wilabuzu Ludigija amesema uboreshwaji wa haki za binadamu ni hatua muhimu katika kutuletea maendeleo na hatua ambazo Tanzania imepiga katika maeneo mbalimbali ni kutokana na juhudi kubwa zinazofanywa na Taasisi zinazohusika na haki za kibinadamu kwa kushirikiana na serikali na wadau wengine.

Aidha amesema maadhimisho ya siku ya Haki za Binadamu na Maadili Nchini yanafanyika ili kuwakumbusha na kuwapa elimu wananchi waweze kutambua haki zao na namna wanaweza kupata msaada

" Tunapoazimisha siku hii lengo ni kuwakumbusha na kuwapa elimu wananchi kutambua kwamba serikali bado imeendelea kuvitumia vyombo hivi vitatu ambavyo ni TAKUKURU, Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora, na Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma kwa sababu vyombo hivi vimekuwa vikitusaidia sana kuhakikisha haki inapatikana na inatendeka, kila mtu ambaye anahusishwa kwenye mgogoro ambao upo anapata haki yake stahiki" Amesema Bw.Ludigija

Naye, Afisa Mfawidhi THBUB Tawi la Dar es Salaam, Bi Shoma Philip amesema wadau wa Haki za Binadamu, Maadili na Rushwa wamekutana kwa lengo la kujadili changamoto ambazo wanakumbana nazo katika maeneo ya kazi ambapo zitajadiliwa na kuzipatia ufumbuzi ili kufanya kazi kwa ufanisi na kuweza kuwapatia wananchi haki zao bila upendeleo.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com