WIZARA YA HABARI, MAWASILIANO NA TEKNOLOJIA YA HABARI YATOA MAFUNZO YA ANWANI ZA MAKAZI KWA WAFANYABIASHARA DODOMA

 


Na  Dotto Kwilasa,DODOMA

SERIKALI kupitia Wizara ya habari, mawasiliano na Teknolojia ya habari imekutana na wafanyabiasha wa Jiji la Dodoma kuwapa mafunzo kuhusu umuhimu wa  utekelezaji wa mfumo wa anwani za makazi utakaosaidia kuinua uchumi kidigitali

Hayo yameelezwa  leo Jijini hapa na mtaalamu wa Tehama, Wizara ya ardhi,Nyumba na maendeleo ya makazi Anord Mkude kwenye kikao kazi kati ya Wizara ya habari , mawasiliano na Teknolojia ya habari na wafanyabiasha wa Jiji la Dodoma kuhusu umuhimu wa  utekelezaji wa mfumo wa anwani za makazi.

Amesema umuhimu wa utekelezaji wa mfumo wa anwani za makazi nchini,Mkude alisema unawezesha mipango na tafiti kufanyika kwa tija, kuongeza vyanzo vya fedha , kuimarisha usalama ,kuwezesha utoaji , upatikanaji na upelekaji  wa huduma za bidhaa hadi mahali husika.

Ametaja manufaa mengine kuwa ni kusaidia wawekezaji kufanya maamuzi kabla ya kuamua kufanya uwekezaji na   kuwezesha biashara mtandao kufanikiwa hali itakayo inua fursa ya uchumi wa kidigitali.

Pamoja na hayo ametumia nafasi hiyo kueleza muundo wa anwani za makazi kwa upande wa vijijini kuwa unahusisha namba ya nyumba au jengo,jengo la kitongoji au shehia na namba maalumu ya postikodi na kwa upande wa Miji,muundo wa anwani za makazi unahusisha namba ya nyumba ,jina la mtaa au barabara,namba ya kata au postikodi.

"Jamii inapaswa kutambua kuwa postikodi ni utaratibu wa kitaalam unaotumika kutenga maeneo ya makazi wakati amwani za makazi ni miundombinu ambayo Kwa Pamoja inatambulisha mahali halisi mtu ama kitu kilipo,aina hii ya utambulisho inaundwa na vitu vikuu vitatu ambavyo ni namba ya anwani,jina la barabara na postikodi,"amefafanua 

Mkude amesema,ili kupata tija iliyokusudiwa Katika uanzishwaji wa anwani za makazi na postikodi kila mdau wa maendeleo ana jukumu la kutekeleza kujiwekea miundombinu ya mfumo wa anwani za makazi ikiwa ni pamoja na kutambulisha barabara Kwa kutumia anwani za makazi.

Amesema wananchi pia wanapaswa kuwajibika  kutoa na kupokea huduma Kwa kutumia mfumo wa anwani za makazi na kuhakiki taarifa za mfumo huo  mara kwa mara .

Kwa upande wake Kaimu Katibu tawala Mkoa wa Dodoma Aloyce Mhogofi amesema kikao kazi hicho ni muhimu kwa kuwa kinalenga kujenga uelewa wa pamoja katika kuhamasisha matumizi  ya anwani za makazi na kueleza kuwa wananchi hususani wafanyabiasha wanapaswa kutumia mfumo wa anwani za makazi kuwezesha mafanikio ya kijamii na kiuchumi kufanisi maendeleo Kwa wakati.

Amesema ikiwa  wafanyabiasha watatumia mfumo huo utawawezesha  kukutana na wateja wengi na kuwanufaisha kiuchumi.

"Kundi hili ni muhimu linapaswa kupewa maelezo,ujuzi,taarifa muhimu Kwa ajili ya kufanikiwa kibiashara ,lazima tuelewe kuwa maendeleo ya biashara yanayegemea zaidi mfanyabiashara anayejitambua na kukubali kwenda na wakati,"amesema.


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com
Previous Post Next Post