******************
NA EMMANUEL MBATILO, DAR ES SALAAM
KLABU ya Yanga imeendelea kuonesha makali yake kwenye ligi kuu Tanzania bara baada ya leo kufanikiwa kuichapa Polisi Tanzania kwa mabao 3-0, mchezo ambao ulipigwa kwenye dimba la Benjamin Mkapa Jijini Dar es Salaam.
Kipindi cha kwanza Yanga haikufanikiwa kupachika bao lolote licha ya kupata nafasi nyingi za wazi ambazo hazikuweza kutendewa haki na wachezaji wa Yanga.
Mabao ya Yanga yamefungwa na nyota wao Jesus Moloko, Fiston mayele na bao la tatu lilifungwa na Clement Mzize na kufunga mahesabu ya mabao 3-0 kwenye mchezo huo ambao ulikuwa na burudani ya kutosha.
Social Plugin