Waziri wa maji Jumaa Aweso akizungumza wakati wa ziara yake Jijini Tanga ya kuangalia hali ya upatikanaji wa huduma ya maji safi kwa wananchi
Waziri wa maji Jumaa Aweso akizungumza wakati wa ziara yake Jijini Tanga ya kuangalia hali ya upatikanaji wa huduma ya maji safi kwa wananchi
Mkurugenzi wa Bonde la Mto Pangani Segule Segule akizungumza wakati wa ziara hiyo
Mkurugenzi wa Tanga Uwasa Mhandisi Geofrey Hilly akieleza hatua walizochukua kuondosha changamoto hiyo
Waziri wa Maji Jumaa Aweso katika mwenye kofia akikagua maji katika mtambo wa kusafishia maji wa Mowe Jijini Tanga wakati wa ziara yake
Waziri wa Maji Jumaa Aweso akiwa kwenye mtaa wa Chumbageni Jijini Tanga akikagua upatikanaji wa maji kwa wananchi wakati wa ziara yake
Na Oscar Assenga,Tanga
Waziri wa maji Jumaa Aweso amelazimika kutua Mkoani Tanga kwa ajili ya kufuatilia uwepo wa changamoto ya kukosekana kwa huduma ya maji huku akiitaka Mamlaka ya Maji Safi na Usafiri wa Mazingira (Tanga Uwasa) kuhakikisha taarifa zinatolewa kwa wakati kwa wananchi inapojitokeza hitilafu ya ukosefu wa huduma hiyo muhimu ili kuondoka malalamiko kwao.
Sambamba na hayo aliagiza Bonde la Maji la Mto Pangani kufanya ufuatiliaji kwa wote wanaofanya shughuli za kibinadamu karibu na vyanzo vya maji na hatua kali kuchukuliwa dhidi yao ili kuhakikisha wanakomesha vitendo vya watu kufanya shughuli zao
Akizungumza wakati wa ziara yake ya siku moja Jijini Tanga kuangalia hali ya upatikanaji wa huduma ya Maji kwa wananchi kufuatia changamoto ya ukosefu wake kwa baadhi ya wananchi kwa siku nne mfufulizo chanzo kikitajwa ni uchafuzi wa mazingira uliofanywa na wananchi wanaoishi karibu na vyanzo vya maji vya Mto Zigi hali iliyopelekea maji kuwa katika hali ya uchafu usio kawaida na hivyo kuifanya mamalaka hiyo kusitisha huduma kwa wananchi ili kutatua changamoto hiyo.
Waziri Aweso alisema jukumu la utoaji wa huduma ya maji safi na salama kwa jiji la Tanga ni la Tanga Uwasa ni kuhakikisha wananchi wanapata huduma ya maji hivyo ni kwa nini wananchi walipata huduma ya maji isiyo ya kawaida baada ya kuona maji katika hali ile waliamua kuzima mitambo kwahiyo kelele za watu kukosa maji yaliyokuwa yanapatikana zilileta taharuki pamoja na changamoto iliyojitokeza watu wa maabara na wataalamu wameweza kuyatibu na sasa hivi yapo katika hali yake na tumepita kwa wananchi baadhi ya nyumba maji yapo.
Alisema kubwa ambalo alitaka kusisisitiza kwao ni kwamba inapotokea changamoto kukosekana kwa maji sio jambo baya lazima watoe taarifa kwa wakati na hivyo kutokuitoa kunapelekea tahatuki kwa wananchi hivyo jambo hilo waangalie na lisiitokeze tena .
“Lakini Tanga Uwasa utoaji wa huduma ya majisafi na salama ni wajibu na majukumu ya mamlaka yenu kwahiyo lazima mjipange kuhakikisha mnatoa huduma ya maji safi na salama wakati wote “Alisema Waziri Aweso
“Ndugu zangu maji hayana mbadala lakini pamoja na kurejea huduma hii lazima iundwe timu maalum ya kupita kila mtaa kuona huduma ya maji inarejea kama kawaida yake nina imani hili jambo haliwezi kutokea tena"
Aidha waziri Aweso ameitaka bodi ya mamlaka hiyo kukaa na kujadili namna watakavyoweza kupambana na kutatua changamoto zinazopelekea kukosekana kwa maji akiitaka pia kufanya kikao cha pamoja na madiwani na wenyeviti wa mitaa kuwaeleza hali halisi ya utekelezaji wake hii ikilenga hasa kuweka wazi taarifa za kiutendaji zitakazosaidia kuondoa malalamiko kutoka kwa wananchi.
Akieleza changamoto iliyopelekea kukosekana kwa huduma ya maji kwa siku kadhaa mkurugenzi wa mamlaka ya maji safi na usafi wa mazingira Tanga uwasa Geofrey Hilly alisema kuwa kumekuwa na changamoto ya baadhi ya wananchi kufanya shughuli zao ikiwemo uchimbaji wa madini katika chanzo kibwa cha Mto Zigi kinachotegemewa na mamlaka hiyo hali iliyopelekea kuchafuka kwa maji.
"Tumekuwa na changamoto ya upungufu wa maji tangu mwezi wa 10 mwaka 2022 changamoto kubwa ilikuwa ni upungufu wa umeme katika maeneo yetu ya kuzalisha maji lakini hivi karibuni ikatokea changamoto ya kuchafuka sana kwa maji na imetokana na hali ya uchafuzi wa mazingira katika chanzo chetu kikubwa cha mto Zigi na hata usafishaji wake ulikuwa ni wa hali ngumu kwahiyo tukazima kwanza maji yasije tuyatibu na tumefanikiwa na hivyo tayari maji yameshaanza kutoka kwa baadhi ya maeneo"
Hilly alisema kuwa Mamlaka hiyo ipo mbioni kupambana na changamoto mbalimbali zinazojitokeza mara kwa mara ambapo wamejipanga kununua mitambo maalumu ya kudhibiti changamoto ya kupungua kwa umeme , kupatikana kwa mradi mkubwa wa kujenga tanki la kuhifadhia maji ambapo hata itakapotokea changamoto ya umeme bado maji yatakuwa yanapatikana kwa uhakika.
Hata hivyo kwa upande wake Mkurugenzi wa Bonde la Mto Pangani Segule Segule amekiri uwepo wa baadhi ya wananchi wanaofanya shughuli zao karibu na vyanzo vya maji licha ya jitihada wananzozifanya akiahidi kupokea na kwenda kutekeleza maagizo ya waziri wa Maji Jumaa Aweso.
Alisema bonde hilo ndio lenye dhamana ya kuhakikisha kuwa wenzao wanaochukuwa maji kwenye vyanzo yana kuwa kwenye ubora stahiki hivyo wamezingatia maelekezo ya viongozi na wameshajipanga kutekeleza na wamekuwa wakichukua hatua mbalimbali kwa kushirikiana na madiwani serikali za wilaya na mikoa.
Akizungumza Katibu wa Chama cha Mapinduzi mkoa wa Tanga Suleiman Mzee ameipongeza Tanga Uwasa kwa jitihada za haraka ilizozifanya kutatua changamoto ya kuchafuka kwa maji hali iliyoleta kwa wakazi wa jiji la Tanga kwa siku nne mfululizo huku akiwataka wananchi kuendelea kutunza na kuvilinda vyanzo vya maji vilivyopo.
Akizungumza mmoja wa madiwani wa Jiji la Tanga Salimu Perembo ameishauri mamlaka hiyo kupanua huduma zake kwa upande wa majitaka hii ikienda sambamba na ongezeko la wananchi na makazi ili kuondoa usumbufu unaoweza kujitokeza.
Mamlaka ya maji safi na usafi wa Mazingira inazihudumia wilaya za Tanga Pangani pamoja na Muheza ikiwa inazalisha lita zaidi ya 30 za maji kwa siku ambapo sasa inatekeleza mradi unaogharimu shilingi Billion 9.18 ambao mara baada ya kukamilika utaiwezesha Tanga uwasa kuwa na uhakika maji ya kutosha kwa mahitaji ya wananchi.
Social Plugin