Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

WANANDOA WAFARIKI WAKIPATA JOTO KWENYE JIKO LA MKAA


Watu wawili, wanandoa wamekutwa wamepoteza maisha siku ya Jumanne katika nyumba moja, jimbo la kaskazini mwa Nigeria la Kano kwa kudaiwa kuvuta hewa kaboni monoksidi iliyotokana na kutumia jiko la mkaa, polisi walisema katika taarifa yao.


Mkaa unapochomwa, miongoni mwa gesi nyinginezo, hutoa sumu ya kaboni monoksidi ambayo inapovutwa kwa muda mrefu, hasa katika sehemu zisizo na uingizaji hewa mzuri, inaweza kusababisha kifo.


"Maafisa wetu walipotembelea eneo la tukio waliwapata wanandoa hao wamepoteza maisha na pia harufu ya mkaa ambayo inaashiria kuwa waliitumia jiko la mkaa ili kujiepusha na baridi ya harmattan," taarifa hiyo ilisema.


Msimu wa baridi wa harmattan unaendelea kati ya Novemba na katikati ya Machi. Ni wakati ambao una sifa ya upepo mkali na vumbi kutoka kaskazini-mashariki unaovuma kutoka jangwa la Sahara.

Katika baadhi ya maeneo hii husababisha hali ya hewa ya baridi kali.


Chanzo: BBC SWAHILI

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com