Meneja wa EWURA Kanda ya Ziwa, George Mhina (kushoto) na wanafunzi wa shule ya Sekondari Kabela Gold wakifungua maji kupitia mradi wa maji uliotekelezwa na Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Mjini Kahama (KUWASA) kwa ufadhili wa EWURA.
Na Kadama Malunde – Malunde 1 blog
Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA) imeridhishwa na utekelezaji wa mradi wa kusogeza maji safi katika shule za Sekondari Kabela Gold, Mwime, Bugisha na Kituo cha watoto wenye mahitaji maalum cha Mama Kalembe uliotekelezwa na Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Mjini Kahama (KUWASA).
Akizungumza leo Jumanne Januari 31,2023 wakati akikagua na kuona utekelezaji wa mradi huo wa maji, Meneja wa Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA) Kanda ya Ziwa George Mhina amesema EWURA inaipongeza na kuishukuru KUWASA kupeleka huduma ya maji safi katika shule hizo.
Mhina amesema Mradi huo unatokana na KUWASA kuwa Mamlaka ya Pili Kitaifa kwa ngazi ya Mamlaka za Maji Safi na Usafi wa mazingira za mikoa kwa kutoa huduma bora ya maji safi mwaka 2022 ambapo EWURA iliipongeza na kuipatia KUWASA zawadi ya shilingi Milioni 15 kwa lengo la kurudisha zawadi hiyo kwa jamii kwa kuwapatia huduma ya maji safi.
“EWURA tumekuja kuthibitisha kama kweli KUWASA wamepeleka maji kwenye maeneo tuliyokubaliana na kama kweli huduma ya maji inapatikana. Mradi huu unaotokana fedha za ufadhili wa EWURA ni matokeo ya ushindi wa KUWASA kushika nafasi ya pili kitaifa kwa kutoa huduma bora ya maji safi. Tukakubaliana zawadi hii irudishwe kwa jamii, maji yapelekwe katika shule tatu na kituo kimoja cha watoto wenye mahitaji maalum katika Manispaa ya Kahama”,ameeleza Mhina.
Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Usambazaji Maji na Usafi wa Mazingira wa KUWASA, Mhandisi Magige Marwa amesema utekelezaji wa mradi huo ulianza Juni 2022 na kukamilika Septemba 2022 na unaendelea kutoa huduma huku wanufaika wakiwa zaidi ya 2000.
"EWURA ilitupa zawadi ya shilingi Milioni 15 ambapo nasi EWURA tuliongeza shilingi Milioni 5.3 kwa ajili ya kusogeza huduma ya maji safi kwenye shule hizo tatu na kituo cha watoto wenye mahitaji maalum. Tunashukuru tumekamilisha mradi na huduma ya maji inaendelea kutolewa. Tunaomba walinde miundombinu hii ya jamii", amesema Mhandisi Marwa.
“Tayari wanafunzi, walimu wameanza kupata huduma ya maji safi na salama. KUWASA inatoa wito kwa wananchi ambako mabomba ya maji yamepita waombe huduma ya maji ili kuondokana na adha ya kufuata maji umbali mrefu”, ameongeza Mhandisi Marwa.
Mkuu wa Shule ya Sekondari Bugisha, Musa Mpena na Mwalimu Mshauri Nasaha na Miradi shule ya Sekondari Kabela Gold Bi. Magreth Sikujua wameishukuru EWURA na KUWASA kwa kuwasogezea huduma ya maji safi ambayo wanayatumia kwa shughuli mbalimbali ikiwemo, kunywa,umwagiliaji miti na usafi shuleni.
Nao baadhi ya wanafunzi wa shule hizo, Abubakar Sadick, Rebeca Gwanchele, Fatuma Nyakalugu na Japhet Mwinula wamesema sasa wameondokana na adha ya kutumia muda mrefu kutafuta maji ambayo wala hayakuwa salama, mahudhurio ya wanafunzi darasani yameongeza na wameboresha usafi wa mwili na mazingira shuleni.
Wanafunzi wa shule ya Sekondari Kabela Gold wakifungua maji. Kushoto ni Meneja wa Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA) Kanda ya Ziwa George Mhina.
Meneja wa Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA) Kanda ya Ziwa George Mhina akielezea kuhusu mradi wa maji uliotekelezwa na Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Mjini Kahama (KUWASA) kwa ufadhili wa EWURA

Mkurugenzi wa Usambazaji Maji na Usafi wa Mazingira wa KUWASA, Mhandisi Magige Marwa akielezea kuhusu mradi wa maji uliotekelezwa na Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Mjini Kahama (KUWASA) kwa ufadhili wa EWURA

Mwalimu Mshauri Nasaha na Miradi shule ya Sekondari Kabela Gold Bi. Magreth Sikujua akiishukuru EWURA na KUWASA kwa kupeleka huduma ya maji safi katika shule ya Sekondari Kabela Gold.
Mwanafunzi wa kidato cha nne , Abubakar Sadick akiishukuru EWURA na KUWASA kwa kupeleka huduma ya maji safi katika shule ya Sekondari Kabela Gold.
Mwanafunzi wa kidato cha nne , Rebeca Gwanchele akiishukuru EWURA na KUWASA kwa kupeleka huduma ya maji safi katika shule ya Sekondari Kabela Gold.
Wanafunzi wa shule ya Sekondari Bugisha katika Manispaa ya Kahama wakifungua maji kupitia mradi wa maji uliotekelezwa na Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Mjini Kahama (KUWASA) kwa ufadhili wa EWURA.

Mkuu wa Shule ya Sekondari Bugisha, Musa Mpena akiishukuru EWURA na KUWASA kupeleka huduma ya maji katika shule hiyo.
Meneja wa Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA) Kanda ya Ziwa George Mhina akizungumza katika shule ya Sekondari Bugisha katika Manispaa ya Kahama.
Picha zote na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Social Plugin