Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (mwenye tai nyekundu katikati) akiondoka katika Tangi la maji la Buchama - Tinde.
Na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango ameweka Jiwe la Msingi la Mradi wa Maji ya Ziwa Victoria kwenye Mji wa Tinde utakaogharimu shilingi Bilioni Bilioni 5.2 utanufaisha wananchi 60,000 katika vijiji 22 vya halmashauri ya wilaya ya Shinyanga.
Dkt. Mpango ameweka jiwe la Msingi la Mradi wa Maji ya Ziwa Victoria kwa Mji wa Tinde leo Alhamis Januari 19, 2023 katika Tangi la Maji la Buchama - Tinde Kata ya Tinde wilaya ya Shinyanga.
Akizungumza baada ya kuweka jiwe hilo la Msingi Dkt. Mpango pindi mradi wa maji ya Ziwa Victoria katika Mji wa Tinde na Shelui utaogharimu shilingi Bilioni 24.4 utakapokamilika jumla ya Wananchi 180,000 wa Tinde, Shelui na vijiji jirani watanufaika na mradi huo.
“Sekta ya Maji ni muhimu sana katika kukuza uchumi wa viwanda na kupambana na umaskini, na katika mradi huu wa maji wa Tinde utakuwa na faida kwa wananchi na kuwaepusha kupoteza muda mrefu wa kufuata maji safi salama, pamoja na kutopata magonjwa yatokanayo na matumizi ya maji machafu,”amesema Dkt. Mpango.
Dkt. Mpango utekelezaji wa miradi ya maji ipo kwenye Ilani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Ibara ya 97 na kuahidi kuwa Serikali itaendelea kutekeleza miradi ya maji kwa wananchi kwa sababu maji ni muhimu.
Amesema tangu mwaka 2015 hadi 2019 Jumla ya Miradi ya Maji ambayo Serikali imeitekeleza ni 1,423, vijijini 1,268 na Mijini 155, na kuwataka wananchi waitunze miundombinu ya miradi hiyo pamoja na vyanzo vya maji kwa kupanda miti ili kulinda uoto wa asili.
“Napenda kuwakumbusha wananchi kushirikiana kutunza miundo mbinu ya maji na kutunza mazingira kwa kupanda miti na maua kwenye maeneo yetu ili kunusuru nchi yetu iliyoathiriwa na ukataji miti bila kupanda mipya. Nataka miti mingi zaidi ipandwe hapa tulipo. Ni lazima turejeshe uoto wa asili, hili suala la kuhifadhi mazingira kwenye vyanzo vya maji ni lazima, ni lazima tulinde vyanzo vya maji. Uharibifu wa vyanzo vya maji ni hatari, tutunze vyanzo vya maji, msione Ziwa Victoria ni kubwa linaweza kukauka, tukikosa maji tutakufa, tusichukulie kawaida hili”,amesema Dkt. Mpango.
Katika hatua nyingine Dk, Mpango ameviagiza vyombo vya dola, pamoja na Kamati za ulinzi na usalama kuwasaka wale wote ambao wamekuwa wakijihusisha na wizi wa maji wakiwemo wawekezaji wakubwa na kuwachukulia hatua kali ikiwemo kuwatoza faini.
“Lakini wapo watu wanachepusha maji, wanaharibu vyanzo vya maji, Wawekezaji wakubwa waache kuiba maji, bali wachimbe visima vya maji na siyo kutuibia maji, na wale ambao wanachepusha maji waache, wote waliofanya hivyo wabomoe hivyo vizuizi walivyoweka kwani kila mwananchi anahitaji maji. Wizara ya Maji na Bonde mlishughulikie hili.
Kumekuwa na wizi wa maji, kokote nchini hili iwe mwisho, wakubwa acheni kuiba maji, ni ajabu tena wanaoiba maji ni wawekezaji wakubwa na mnawatoza faini ndogo, nawaonya muache, vyombo vya usalama vifuatilie kubaini wezi wa maji, hao wawekezaji wanaoiba maji wachimbe visima vya maji, wavune maji”,amesema Dkt. Mpango.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango akizungumza na wananchi wa Shinyanga baada ya kuweka Jiwe la Msingi la Mradi wa Maji ya Ziwa Victoria kwenye Mji wa Tinde.
“Nimefurahi kusikia watumishi idara ya maji yamebadilika, lakini masikio yangu kwa wananchi bado kuna malalamiko ya wananchi kubambikiwa bili za maji, na hapa mbadiike, wananchi wanasema wakati mwingine wasoma mita hawasomi mita, wanakadiria, nataka wabadilike, watoe bili kadiri wananchi walivyotumia”, ameongeza Dkt. Mpango.
Dkt. Mpango pia ameagiza Wakaguzi pamoja na Baraza la uhifadhi wa Mazingira (NEMC) kufanya ukaguzi wa mara kwa mara kwenye mabwawa yote ya taka sumu migodini ili kusijetokea tatizo kama lilivyotokea katika bwawa la Mgodi wa Almasi Mwadui.
Wakazi wa Tinde
Pia amemwagiza Mthamini Mkuu wa Serikali kukamilisha uthamini haraka juu wa waathirika wa Tope wa bwawa la Mgodi wa Almasi Mwadui ,ili walipwe fidia zao haraka na kuendelea na maisha yao.
Kwa upande wake, Balozi wa India nchini Tanzania, Bw. Binaya Srikanta Pradhan amesema serikali ya Indi itaendelea kushirikiana na serikali ya Tanzania katika kutekeleza miradi mbalimbali ikiwemo ya maji
Waziri wa Maji Jumaa Aweso, amesema Serikali itaendelea kutekeleza miradi ya maji kwa wananchi na kubainisha kuwa katika Mkoa wa Shinyanga kuna miradi ya maji 18 ya kimkakati ambayo inatekelezwa, na wilaya ya Shinyanga kuna miradi mitatu yenye thamani ya Sh.bilioni 1.9.
Waziri Aweso mradi huo wa Maji ya Tinde unatarajiwa kukamilika ndani ya miezi miwili ambapo wananchi wataanza kupata huduma ya maji safi na salama ingawa tayari maji hayo yameanza kutoka katika mji wa Didia.
Mbunge wa Jimbo la Solwa Mhe. Ahmed Salum, amepongeza utekelezaji wa mradi huo mkubwa wa maji jimboni kwake , na kueleza kuwa katika jimbo hilo lina vijiji 126 na mpaka sasa kutakuwa na vijiji 89 ambavyo vinapata huduma ya maji safi na salama, na kusalia vijiji 37 ambavyo navyo vipo kwenye mchakato wa kupata maji.
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Maji Mhandisi Nadhifa Kemikimba, akisoma taarifa ya Mradi huo wa Maji ya Ziwa Victoria, amesema katika mji huo wa Tinde vitahudumiwa vijiji 22 na kunufaisha wananchi elfu 60, ambapo pia maji hayo yanahudumia na wananchi wa Shelui wilayani Iramba mkoani Singida na una gharama ya Sh.bilioni 24.4.
ANGALIA PICHA HAPA CHINI
Muonekano wa Tangi la Maji la Buchama - Tinde lenye ujazo wa lita 1,150,000
Muonekano wa Tangi la Maji la Buchama - Tinde lenye ujazo wa lita 1,150,000
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Maji Mhandisi Nadhifa Kemikimba, akimwelezea Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango kuhusu Mradi wa Maji ya Ziwa Victoria katika Mji wa Tinde na vijiji jirani wilaya ya Shinyanga Mkoani Shinyanga.
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Maji Mhandisi Nadhifa Kemikimba, akimwelezea Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (kushoto) kuhusu Mradi wa Maji ya Ziwa Victoria katika Mji wa Tinde na vijiji jirani wilaya ya Shinyanga Mkoani Shinyanga.
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Maji Mhandisi Nadhifa Kemikimba, akimwelezea Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango kuhusu Mradi wa Maji ya Ziwa Victoria katika Mji wa Tinde na vijiji jirani wilaya ya Shinyanga Mkoani Shinyanga.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (kulia) akiweka Jiwe la Msingi la Mradi wa Maji ya Ziwa Victoria kwa Mji wa Tinde katika Tangi la maji la Buchama - Tinde.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (kulia) akiweka Jiwe la Msingi la Mradi wa Maji ya Ziwa Victoria kwa Mji wa Tinde katika Tangi la maji la Buchama - Tinde.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (kulia) akiweka Jiwe la Msingi la Mradi wa Maji ya Ziwa Victoria kwa Mji wa Tinde katika Tangi la maji la Buchama - Tinde.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango akipanda mti katika Tangi la maji la Buchama - Tinde.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango akimwagilia maji kwenye mti aliopanda katika Tangi la maji la Buchama - Tinde.
Muonekano wa mti wa Mzaituni uliopandwa na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango katika Tangi la maji la Buchama - Tinde.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (mwenye tai nyekundu katikati) akiondoka katika Tangi la maji la Buchama - Tinde.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (mwenye tai nyekundu katikati) akiondoka katika Tangi la maji la Buchama - Tinde.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango akisalimiana na kikundi cha ngoma ya Kisukuma
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango akizungumza na wananchi wa Shinyanga baada ya kuweka Jiwe la Msingi la Mradi wa Maji ya Ziwa Victoria kwenye Mji wa Tinde
Waziri wa Maji Jumaa Aweso akizungumza baada ya Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango kuweka Jiwe la Msingi la Mradi wa Maji ya Ziwa Victoria kwenye Mji wa Tinde
Waziri wa Maji Jumaa Aweso akizungumza baada ya Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango kuweka Jiwe la Msingi la Mradi wa Maji ya Ziwa Victoria kwenye Mji wa Tinde
Msanii Mrisho Mpoto akitoa burudani baada ya Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango kuweka Jiwe la Msingi la Mradi wa Maji ya Ziwa Victoria kwenye Mji wa Tinde
Balozi wa India nchini Tanzania, Bw. Binaya Srikanta Pradhan akizungumza baada ya Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango kuweka Jiwe la Msingi la Mradi wa Maji ya Ziwa Victoria kwenye Mji wa Tinde
Naibu Waziri wa Afya Dkt. Godwin Mollel akizungumza baada ya Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango kuweka Jiwe la Msingi la Mradi wa Maji ya Ziwa Victoria kwenye Mji wa Tinde
Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Shinyanga Mhe. Mabala Mlolwa akizungumza baada ya Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango kuweka Jiwe la Msingi la Mradi wa Maji ya Ziwa Victoria kwenye Mji wa Tinde
Mbunge wa Jimbo la Solwa Mhe. Ahmed Salum akizungumza baada ya Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango kuweka Jiwe la Msingi la Mradi wa Maji ya Ziwa Victoria kwenye Mji wa Tinde
Kaimu Mkuu wa Mkoa Dkt. Yahaya Nawanda akizungumza baada ya Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango kuweka Jiwe la Msingi la Mradi wa Maji ya Ziwa Victoria kwenye Mji wa Tinde
Kwaya kutoka Wizara ya Afya ikitoa burudani
Kwaya kutoka Wizara ya Afya ikitoa burudani
Mrisho Mpoto akitoa burudani