Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Dkt. Yahaya Nawanda akitoa taarifa kwa vyombo vya habari kuhusu ziara ya Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Philip Mpango leo Jumanne Januari 17,2023 kwenye Hospitali mpya ya Rufaa Mkoa wa Shinyanga iliyopo Mwawaza katika Manispaa ya Shinyanga. Picha na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Dkt. Yahaya Nawanda akitoa taarifa kwa vyombo vya habari kuhusu ziara ya Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Philip Mpango.
Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Dkt. Yahaya Nawanda akitoa taarifa kwa vyombo vya habari kuhusu ziara ya Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Philip Mpango leo Jumanne Januari 17,2023 kwenye Hospitali mpya ya Rufaa Mkoa wa Shinyanga.
Na Kadama Malunde – Malunde 1 blog
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Philip Mpango anatarajiwa kufanya ziara Mkoani Shinyanga ambapo miongoni mwa shughuli atakazofanya ni pamoja na kuweka Jiwe la Msingi Hospitali ya Mpya ya Rufaa ya Mkoa wa Shinyanga iliyopo katika kata ya Mwawaza Manispaa ya Shinyanga.
Akitoa taarifa kwa vyombo vya habari leo Jumanne Januari 17,2023 akiwa kwenye Hospitali ya Rufaa Mkoa wa Shinyanga, Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Dkt. Yahaya Nawanda amesema uwekaji wa jiwe la msingi katika hospitali hiyo inayoendelea kujengwa utafanyika kesho Jumatano Januari 18,2023.
“Akiwa mkoani Shinyanga Mhe. Makamu wa Rais Dkt. Philip Mpango kesho asubuhi atakuwa Isaka wilayani Kahama ambapo ataweka jiwe la msingi Ujenzi wa kipande cha nne cha Reli ya Kisasa (SGR) cha Isaka – Tabora lakini pia mchana atakuja kuweka jiwe la msingi katika hospitali ya rufaa ya Mkoa wa Shinyanga ambayo tayari imeanza kutoa huduma za afya na Januari 19,2023 ataweka jiwe la msingi ujenzi wa mradi wa maji Tinde – Shelui”,amesema Dkt. Nawanda.
Dkt. Nawanda ambaye pia ni Mkuu wa Mkoa wa Simiyu amewaomba wakazi wa Shinyanga kujitokeza kwa wingi kumpokea Mhe. Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Philip Mpango na kushuhudia uwekaji mawe ya msingi kwenye miradi hiyo.