ANUSURIKA KUTAFUNWA NA MAMBA AKIOSHA UTUMBO WA NGURUWE MTONI


Paulo Mapunda (54) Mkazi wa Kijiji cha Kipingu Kata ya Ruhuhu Wilaya ya Ludewa Mkoani Njombe amenusurika kufa baada ya kushambuliwa na Mamba wakati akisafisha utumbo wa nguruwe kandokando ya Mto Ruhuhu na kumkata mguu wake wa kulia katika eneo la goti.


Mapunda amesema January Mosi majira ya saa tano asubuhi nyumbani kwake kulikuwa na sherehe ya kipaimara hivyo walichinja nguruwe ambapo yeye alichukua utumbo kwenda kuusafisha Mtoni hapo huku akiwa ndani ya mtumbwi ndipo Mamba akajitokeza na kubinua mtumbwi kisha yeye kuangukia ndani ya maji.


Amesema Mamba alikamata mguu wake wa kulia na kumzamisha kwenye maji lakini alijitahidi kuushikilia mtumbwi huku wakivutana na yeye akipiga kelele za kuomba msaada ndipo Watu walipojitokeza kakini Mamba huyo akamkata mguu wake na kuondoka nao ndipo akaokolewa na kukimbizwa Hospitali ya Peramiho.

Mpaka sasa tayari amepatiwa matibabu ya awali na anatakiwa kufanyiwa upasuaji lakini anashindwa kupata huduma hiyo kutokana na kutokuwa na fedha za kulipia matibabu hayo huku akiiomba Serikali iwapelekee mabomba ya maji kwani mara kwa mara Watu wamekuwa wakijeruhiwa na Mamba.


Mtendaji wa kata hiyo Yusuph Lukuwi amethibisha kutokea kwa tukio hilo huku Mwenyekiti wa Kijiji cha Kipingu Alponce Mbeya akisema baada ya tukio hilo kutokea walikopa fedha mahali kiasi cha Tsh. 700,000 kwa ahili ya gari la Wagonjwa na matibabu ya awali na bado hazikutosheleza hivyo bado kuna uhitaji wa fedha zaidi kwa ajili ya matibabu.


Chanzo: MillardAyo

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post