Na John Walter-Karatu
Mwanamke mmoja mkazi wa kijiji cha Mangola Juu Kata Ya Daa wilayani Karatu mkoani Arusha amefariki dunia baada ya kushambuliwa na mbogo.
Tukio hilo limetokea tarehe 23 Januari mwaka huu wakati mwanamke huyo aitwaye Katarina Ngaida akimsindikiza mtoto wake shule.
Akielezea kuhusu tukio hilo diwani wa kata ya Daa, Alex Martin Sidawe amesema mama huyo alifariki dunia akiwa njiani kupelekwa hospitalini.
Kufuatia tukio hilo diwani wa kata hiyo ameiomba serikali kufungua shule mbili mpya ambazo zimejengwa ili kuwaondolea adha wazazi ya kuwasindikiza watoto kwa kuwa shule ziko mbali.
Social Plugin