Joyce Japhet (5) mtoto mkazi wa kitongoji cha Kilimahewa kata ya Lulembela, wilayani Mbogwe mkoani Geita amenusurika kufa baada ya kushambuliwa na Paka ambaye alimng'ata na kumng'ang'ania usoni mpaka alipokatwa shingo ndipo akamuachia.
Paka huyo anayehusishwa na imani za kishirikina kabla ya kumshambulia mtoto huyo aliwashambulia pia watu wazima wanne katika eneo hilo kwa nyakati tofauti.
"Nilisikia mtoto analia nimeumwa na Paka, baada ya kutoka pale akaja nae mpaka ndani yule mtoto amemshikilia sehemu ya shavu nikaona hivi na mimi nikajitahidi kumnyonga yule paka, ikashindikana mpaka nikatumia kitu kikali yule paka kuchinja", alisema Marco Jopola jirani wa familia ya mtoto huyo.
Mwenyekiti wa kitongoji hicho Katendele Katendele amekiri kutokea kwa matukio ya watu watano kuvamiwa na Paka huyo ambaye baada ya kuchinjwa walimzika na baadae wakamkuta anapumua ndipo wakafikia maamuzi ya kumchoma moto.
Chanzo:EATV
Social Plugin