Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

FUNDI AFARIKI KWA KUCHOMWA NA PANGA AKIKWEPA KUANGUKIWA NA MTI ALIOKUWA ANAUKATA






NA MWANDISHI WETU-SERENGETI MEDIA CENTRE.

Fundi ujenzi Bahati Mkirya (28) mkazi wa Kijiji cha Rung’abure wilayani Serengeti anadaiwa kufa kwa kuchomwa na panga kifuani baada ya kuanguka akikwepa kuangukiwa na mti wa mwembe aliokuwa anakata.



Mwenyekiti wa Serikali ya Kijiji hicho Joseph Meng’anyi amethibitisha tukio hilo ambalo limetokea leo Ijumaa Januari 6,2023 majira ya saa 6 mchana katika Kitongoji cha Kwanina,anadai taarifa kutoka kwa mtoto wake ni kuwa ameangukia panga alilokuwa nalo wakati anakwepa kuangukiwa na mti.



Amesema..."Tumesikia yowe kwenda tukamkuta yuko chini ameishakufa na anajeraha kubwa kifuani,panga likiwa pembeni lina damu na mti wa mwembe uliokuwa jirani na nyumba ya mama yake aliokuwa anakata ukiwa umeanguka chini,”anasema.



Na kwa maelezo ya mtoto wake wa kiume wa miaka 6 aliyekuwepo amesema,baba yake amenguka chini wakati anakimbia asiangukiwe na mti aliokuwa anakata,kisha akaamka na baadae akamwona anaishiwa nguvu anaanguka chini akaenda kumwambia bibi yake.



“Mama wa marehemu alipofika akamkuta ameshakufa akapiga yowe ndipo tukaenda nasi tukakuta hali hiyo,kwa kweli alikuwa na jeraha kubwa kifuani,inaonekana wakati anajaribu kukwepa huo mti akaanguka panga likamchoma na kisha kulitoa na kulitupa pembeni,tumekuta damu zinavuja kwa ndani na nyingine chini,”amesema.


Meng’anyi ameiambia Serengeti Media kuwa ameishajulisha Polisi ili wafike eneo la tukio kwa ajili ya uchunguzi zaidi wa tukio hilo,kwa mjibu wa Polisi wilayani hapa wamekiri kupata taarifa na wameenda eneo la tukio.


Chanzo - Serengeti Media Centre

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com