Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga ACP Janeth Magomi akizungumza na waandishi wa habari leo Jumatatu Januari 23,2023.
Na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Jeshi la Polisi Mkoa wa Shinyanga limekamata, mali za wizi, dawa za kulevya pamoja na Pikipiki nane zinazodaiwa kutumika kwa wizi na nyara za serikali yakiwemo maganda ya mayai ya mbuni, mikia ya nyumbu, ngozi na kucha za paka pori, ngozi ya mbuzi mawe na Fungo.
Akitoa taarifa kwa vyombo vya habari leo Jumatatu Januari 23,2023 Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga ACP Janeth Magomi amesema vitu hivyo pamoja na vielelezo vimekamatwa wakati wa misako na doria zilizofanywa na Jeshi la Polisi Mkoa wa Shinyanga kwa kipindi cha mwezi mmoja kuanzia Desemba 20,2022 hadi Januari 23,2023.
“Tumefanikiwa kukamata pikipiki 8 zilizokuwa zinatumika kwa wizi au za wizim bangi kilo 10,kete 278. Vitu vingine ni nyara za serikali ambazo ni mikia 21 ya nyumbu, maganda 5 ya mayai ya mbuni,ngozi moja ya paka pori, kipande kimoja ca ngozi ya mbuzi mawe, miiba 44 ya nungunungu, vipande vitatu vya mkonga wa tembo, mikia 3 ya ngiri,vipande 3 vya magamba ya kobe,kucha 5 za paka pori,kipande kimoja cha jino la tembo, kipande kimoja cha ngozi ya fungo na kipande kimoja cha pembe ya korongo”,amesema Kamanda Magomi.
“Vile vile tumekamata meter 1 ya TANESCO, Solar panel 1,control box 1 ya mtambo, Tv 4, Subwoofer 1, mafuta ya petrol lita 225, bidhaa mbalimbali za dukani, seti moja ya muziki wa Disco, Pombe kali aina mbalimbali, pombe ya moshi lita 10,computer 1, godoro 1, viti 10 vya plastic, nyaya za miundombinu ya mawasiliano ya TTCL, battery 2 kubwa za gari, vyuma vya miundombinu ya barabara, madumu 42 yaliyotaka kutumika katika wizi wa mafuta kwenye Ujenzi wa mradi wa Reli ya Kisasa katika eneo la Seke wilayaNI Kishapu”,ameeleza Kamanda Magomi.
Kamanda Magomi amesema pia Jeshi la Polisi liliokota pikipiki 9 ambazo zinadaiwa kusahaulika au kutupwa katika maeneo mbalimbali kutokana na sababu tofauti kama vile uhalifu na ulevi.
Kamanda huyo wa Polisi amewataka wananchi kuacha vitendo vya uhalifu na washirikiane na Polisi katika kutokomeza uhalifu na kuacha kujichukulia sheria mkononi kwa kuwaadhibu wahalifu na badala yake kuwafikisha katika vituo vya polisi kwani kitendo hicho ni kosa la jinai na linahatarisha usalama wa raia.
Jeshi la polisi mkoa wa Shinyanga linawataka wananchi kufika katika kituo kikuu cha Polisi Mkoa wa Shinyanga kwa ajili ya kutambua mali mbalimbali zilizokamatwa kuanzia Januari 23,2023 hadi Januari 30,2023.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga ACP Janeth Magomi akizungumza na waandishi wa habari leo Jumatatu Januari 23,2023.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga ACP Janeth Magomi akizungumza na waandishi wa habari leo Jumatatu Januari 23,2023.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga ACP Janeth Magomi akizungumza na waandishi wa habari leo Jumatatu Januari 23,2023.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga ACP Janeth Magomi akizungumza na waandishi wa habari leo Jumatatu Januari 23,2023.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga ACP Janeth Magomi akionesha vifaa vilivyokamatwa na jeshi la polisi
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga ACP Janeth Magomi akionesha nyara za serikali walizokamata
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga ACP Janeth Magomi akionesha seti moja ya muziki wa Disco waliyokamata
Seti ya muziki wa Disco iliyokamatwa
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga ACP Janeth Magomi akionesha mali walizokamata
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga ACP Janeth Magomi akionesha mali walizokamata
Miundombinu ya TTCL na barabara
Mali zilizokamatwa
Mali zilizokamatwa
Nyara za serikali na vifaa vya kufanyia uganga
Muonekano wa pikipiki zilizokamatwa
Social Plugin