Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

KAZI IMEANZA, HAKUNA KUSUBIRI....TAYARI SOPHIA MJEMA KATUA LUMUMBA


Katibu wa Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi Taifa (NEC) Idara ya Itikadi na Uenezi Ndugu Sophia Edward Mjema amewasili Ofisini kwake Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, Lumumba Dar es Salaam leo Jumatatu tarehe 16 Januari, 2022.


 Akizungumza na watumishi na maafisa wa idara yake, Ndugu Mjema amewataka kutekeleza majukumu yao kwa bidii, umoja, ubunifu na wakati wote kuhakikisha wanakuwa mfano bora katika kuendelea kujenga, kutunza na kulinda haiba nzuri ya CCM na Mwenyekiti wake Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan.


Amesisitiza kazi kubwa iliyopo mbele ni kuendelea kuyasema mazuri yanayofanyika kwa wananchi ili wayafahamu, kueleza uzuri wa CCM, kuwasikiliza wananchi kero au changamoto zao ili kuzitafutia ufumbuzi, kufuatilia utekelezaji wa ilani ya uchaguzi na kuendelea kuwajengea uwezo wanachama na viongozi wetu kupitia mafunzo. Kazi zote hizi hazipaswi kusubiri, tuanze sasa na tuendelee mbele.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com