UWT SHINYANGA MJINI WAADHIMISHA MIAKA 46 YA CCM KWA KUTEMBELEA HOSPITALI YA RUFAA SHINYANGA, KAMBARAGE NA WATOTO WENYE UALBINO...MAJESHI AWALIPUA VIONGOZI CCM.."BADO KUNA NONGWA UBUNGE"



Na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Jumuiya ya Umoja wa Wanawake (UWT) Wilaya ya Shinyanga Mjini imeadhimisha Miaka 46 ya kuzaliwa kwa Chama cha Mapinduzi (CCM) kwa kutembelea Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Shinyanga, Kituo cha Afya Kambarage, Kituo cha Watoto wenye mahitaji maalum (viziwi,wasioona na wenye ualbino) cha Buhangija, kupanda miti pamoja na kuzungumza na wananchi wa kata ya Masekelo Manispaa ya Shinyanga.

Maadhimisho hayo yamefanyika leo Jumapili Januari 29,2023 ambapo Mgeni rasmi alikuwa Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Shinyanga Mjini, Mhe. Anord Makombe.

Akizungumza wakati wa maadhimisho hayo, Makombe amewaomba wananchi kuendelea kuiamini Serikali ya CCM kutokana na jitihada kubwa inazozifanya katika kuwaletea maendeleo wananchi kwa kutekeleza miradi mbalimbali.

“Tunapotimiza miaka 46 ya CCM naomba wananchi muendelee kuiamini serikali ya CCM inayoongozwa na Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan ambayo imekuwa ikileta fedha nyingi kwa ajili ya maendeleo katika sekta mbalimbali ikiwemo afya, elimu, miundombinu n.k. Nimepita katika kituo cha watoto wenye mahitaji maalumu cha Buhangija ujenzi wa mabweni unaendelea baada ya Mhe. Rais Samia kuleta fedha kiasi cha shilingi Milioni 190 zilizotakiwa zitumike maadhimisho ya Uhuru”,amesema Makombe.

“CCM imefanya mambo mengi yanayoonekana kwa macho, serikali imewekeza fedha nyingi, endeleeni kuiamini CCM, ipo kazini kuhakikisha inatatua matatizo ya wananchi”,ameeleza Makombe.

Aidha ametumia fursa hiyo kuwataka viongozi wa serikali za mitaa na watendaji wa kata kuhakikisha watoto wote wanakwenda shule huku pia akihamasisha wazazi kupeleka watoto shule na kuwalinda dhidi ya vitendo vya ukatili wa kijinsia kama vile ubakaji,ulawiti na usagaji.

“Tutashughulika na wenyeviti wa mitaa na watendaji wa kata, shule zimeongezeka, wanafunzi wote walioandikishwa kujiunga kidato cha kwanza lazima waende shule. madarasa yapo ya kutosha hivyo tunataka watoto wasome na walindwe dhidi ya vitendo vya ukatili”,amesema Makombe.
Kaimu Mganga Mfawidhi Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Shinyanga Dkt. Mwita Chacha (mwenye suti nyeusi) akielezea kuhusu mashine ya CT - Scan iliyopo katika hospitali hiyo.

Kwa upande wake, Mwenyekiti wa UWT Wilaya ya Shinyanga Mjini Mhe. Rehema Nhimanilo na Katibu wa UWT Wilaya ya Shinyanga Mjini Mhe. Ruth Enock wamesema wameamua kuadhimisha miaka 46 ya CCM kwa kutoa misaada mbalimbali ikiwemo sabuni na mafuta kwa watoto wanaolelewa katika kituo cha Buhangija pamoja na kwa akina mama waliojifungua katika Kituo cha Afya Kambarage sambamba na kupanda miti katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Shinyanga iliyopo Mwawaza.

Hata hivyo, Katibu wa CCM Wilaya ya Shinyanga Mjini, Ally Majeshi amesema wanapoadhimisha Miaka 46 ya kuzaliwa kwa CCM viongozi wa Chama cha Mapinduzi na wale waliopewa ridhaa kwa tiketi ya CCM ni lazima wawe wakomavu wa siasa, mtu asitumie cheo chake kutengeneza maneno maneno na malumbano ndani ya chama hicho.
Katibu wa CCM Wilaya ya Shinyanga Mjini, Ally Majeshi akizungumza kwenye mkutano wa hadhara katika kata ya Masekelo Manispaa ya Shinyanga.

“Tunapotimiza miaka 46 bado kuna maeneo na watu, ndani ya CCM kuna watu wanadhani chama hiki kina miaka minane hawa wanatakiwa wapimwe na madaktari. Bado ndani ya CCM tuna nongwa za uchaguzi. Tuna nongwa za uchaguzi wa serikali za mitaa 2019, kura za maoni kuwapata wenyeviti wa serikali za mitaa kwenye mikutano mikuu yao ya chama ya matawi”,amesema Majeshi.

“Wanaojaliwa kuteuliwa kupata nafasi za kupeperusha bendera wanafikiri wamepewa hatimiliki ya hizo nafasi walizopewa au wao ndiyo watu sahihi ndani ya chama jambo ambalo siyo sahihi kabisa, waache, tuwaombe wanachama wetu, viongozi wetu nongwa za uchaguzi ziishe.

Lakini mwenyekiti tulivyotoka mwaka 2019 tukaenda 2020 nongwa za ubunge zipo, tunazo nongwa kwenye hiyo nafasi ya Ubunge. Unapopewa nafasi au ridhaa ndani ya chama ni umepewa nafasi na ridhaa kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi, hujamilikishwa chama, maana yake nini Mwenyekiti? Viongozi wetu waliopewa dhamana wasifanye kazi ya kukigawa chama kwa sababu ya kwamba, kwa kuwa wao wana nafasi basi wale ambao waliomba nao ridhaa hawana thamani na heshima na hadhi ndani ya chama, jambo hili mwenyekiti siyo sahihi”,ameeleza Majeshi.
Wananchi na wanachama wa CCM wakifuatilia mkutano wa hadhara katika kata ya Masekelo Manispaa ya Shinyanga.

“Mwenyekiti nisipoyasema haya tutakuwa tunaendelea kuongoza chama chenye mabaka mabaka na makovu, maajali na matatizo yasiyokuwa na sababu.  Mwaka wa 2022 tumetoka kwenye uchaguzi wa chama na bahati nzuri uchaguzi huo wa 2022 mimi nilikuwa mkurugenzi wa uchaguzi ndani ya chama nawafahamu wanachama na viongozi wanaoendeleza nongwa za uchaguzi, chama hiki chetu wote sisi, aliyepewa nafasi ni chama chake na aliyekosa nafasi naye ni chama chake”,ameongeza Majeshi.

Majeshi amewataka wanachama na viongozi wenye tabia ya kutaka kuivuruga CCM waache.

“Mhe. Mwenyekiti watu waacha tabia za kukivuruga chama kwa sababu ya tafsiri potovu ambazo anakuwa nazo yeye mwenyewe mtu binafsi, haiwezekani mwenyekiti leo tukawa na kiongozi mwenzetu ana jambo lake halafu wanaCCM wakaenda kumsaidia, halafu kiongozi wa chama kama mimi Majeshi nikalalamika kwanini wanachama wameenda kwake, hii siyo sahihi”,amesema Majeshi.

ANGALIA PICHA HAPA CHINI
Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Shinyanga Mjini, Mhe. Anord Makombe (kulia) akizungumza wakati UWT Shinyanga Mjini ikitembelea Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Shinyanga leo Jumapili Januari 29,2023 ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya miaka 46 ya CCM. Picha na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Katibu wa UWT Wilaya ya Shinyanga Mjini Mhe. Ruth Enock ( wa nne kushoto) akizungumza Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Shinyanga
Kaimu Mganga Mfawidhi Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Shinyanga Dkt. Mwita Chacha (mwenye suti nyeusi) akielezea kuhusu majengo yaliyopo katika hospitali hiyo.
Kaimu Mganga Mfawidhi Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Shinyanga Dkt. Mwita Chacha (mwenye suti nyeusi) akielezea kuhusu mashine ya CT - Scan iliyopo katika hospitali hiyo.
Kaimu Mganga Mfawidhi Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Shinyanga Dkt. Mwita Chacha (mwenye suti nyeusi) akielezea kuhusu mashine ya X-Ray iliyopo katika hospitali hiyo.
Kaimu Mganga Mfawidhi Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Shinyanga Dkt. Mwita Chacha (mwenye suti nyeusi) akielezea ujenzi wa majengo unaoendelea katika hospitali hiyo
Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Shinyanga Mjini , Anord Makombe akipanda mti katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Shinyanga

Mwenyekiti wa UWT Wilaya ya Shinyanga Mjini Mhe. Rehema Nhimanilo akipanda mti katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Shinyanga
Mwenyekiti wa UWT Wilaya ya Shinyanga Mjini Mhe. Rehema Nhimanilo akizungumza katika kituo cha Afya Kambarage Manispaa ya Shinyanga
Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Shinyanga Mjini , Anord Makombe akiongozana na viongozi mbalimbali kutembelea majengo ya Kituo cha afya Kambarage
Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Shinyanga Mjini , Anord Makombe na Mwenyekiti wa UWT Wilaya ya Shinyanga Mjini Mhe. Rehema Nhimanilo (kushoto) na Katibu wa UWT Wilaya ya Shinyanga Mjini Mhe. Ruth Enock (kushoto) wakimsalimia na kumpa zawadi ya sabuni mama aliyejifungua katika kituo cha afya Kambarage
Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Shinyanga Mjini , Anord Makombe na Mwenyekiti wa UWT Wilaya ya Shinyanga Mjini Mhe. Rehema Nhimanilo (kulia) na Katibu wa UWT Wilaya ya Shinyanga Mjini Mhe. Ruth Enock (kushoto) wakimsalimia na kumpa zawadi ya sabuni mama aliyejifungua katika kituo cha afya Kambarage

Mwenyekiti wa UWT Wilaya ya Shinyanga Mjini Mhe. Rehema Nhimanilo akimpa zawadi ya sabuni mama mjamzito katika kituo cha afya Kambarage
Mwenyekiti wa UWT Wilaya ya Shinyanga Mjini Mhe. Rehema Nhimanilo akizungumza jambo baada kumpa zawadi ya sabuni mama mjamzito katika kituo cha afya Kambarage
Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Shinyanga Mjini , Anord Makombe na Mwenyekiti wa UWT Wilaya ya Shinyanga Mjini Mhe. Rehema Nhimanilo wakiwa wamebeba mtoto mchanga katika kituo cha afya Kambarage
Zoezi la kukabidhi zabuni likiendelea katika kituo cha afya Kambarage
Viongozi wa CCM na kituo cha afya Kambarage wakipiga picha ya pamoja baada ya kutembelea majengo yanayojengwa
Katibu wa UWT Wilaya ya Shinyanga Mjini Mhe. Ruth Enock  akizungumza katika kituo cha kulelea watoto wenye mahitaji maalum cha Buhangija
Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Shinyanga Mjini , Anord Makombe akizungumza katika kituo cha kulelea watoto cha Buhangija
Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Shinyanga Mjini , Anord Makombe na Mwenyekiti wa UWT Wilaya ya Shinyanga Mjini Mhe. Rehema Nhimanilo (kushoto) wakikabidhi zawadi ya sabuni na mafuta kwa watoto wanaolelewa katika kituo cha Buhangija Manispaa ya Shinyanga

Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Shinyanga Mjini , Anord Makombe na Mwenyekiti wa UWT Wilaya ya Shinyanga Mjini Mhe. Rehema Nhimanilo (kushoto) wakikabidhi zawadi ya sabuni na mafuta kwa watoto wanaolelewa katika kituo cha Buhangija Manispaa ya Shinyanga
Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Shinyanga Mjini , Anord Makombe akizungumza kwenye mkutano wa hadhara katika kata ya Masekelo Manispaa ya Shinyanga
Katibu wa CCM Wilaya ya Shinyanga Mjini, Ally Majeshi akizungumza kwenye mkutano wa hadhara katika kata ya Masekelo Manispaa ya Shinyanga
Katibu wa CCM Wilaya ya Shinyanga Mjini, Ally Majeshi akizungumza kwenye mkutano wa hadhara katika kata ya Masekelo Manispaa ya Shinyanga
Katibu wa UWT Wilaya ya Shinyanga Mjini, Ruth Enock akizungumza kwenye mkutano wa hadhara katika kata ya Masekelo Manispaa ya Shinyanga
Katibu wa UWT Wilaya ya Shinyanga Mjini, Ruth Enock akizungumza kwenye mkutano wa hadhara katika kata ya Masekelo Manispaa ya Shinyanga

Mwenyekiti wa UWT Wilaya ya Shinyanga Mjini Mhe. Rehema Nhimanilo akizungumza kwenye mkutano wa hadhara katika kata ya Masekelo Manispaa ya Shinyanga
Mwenyekiti wa UWT Wilaya ya Shinyanga Mjini Mhe. Rehema Nhimanilo akizungumza kwenye mkutano wa hadhara katika kata ya Masekelo Manispaa ya Shinyanga
Wananchi na wanachama wa CCM wakifuatilia mkutano wa hadhara katika kata ya Masekelo Manispaa ya Shinyanga


Wananchi na wanachama wa CCM wakifuatilia mkutano wa hadhara katika kata ya Masekelo Manispaa ya Shinyanga
Wananchi na wanachama wa CCM wakifuatilia mkutano wa hadhara katika kata ya Masekelo Manispaa ya Shinyanga
Wananchi na wanachama wa CCM wakifuatilia mkutano wa hadhara katika kata ya Masekelo Manispaa ya Shinyanga
Mkutano wa hadhara ukiendelea katika kata ya Masekelo Manispaa ya Shinyanga
Wananchi na wanachama wa CCM wakifuatilia mkutano wa hadhara katika kata ya Masekelo Manispaa ya Shinyanga
Maafisa Maendeleo ya Jamii Manispaa ya Shinyanga na wanachama wa CCM wakifuatilia mkutano wa hadhara katika kata ya Masekelo Manispaa ya Shinyanga
Wananchi na wanachama wa CCM wakifuatilia mkutano wa hadhara katika kata ya Masekelo Manispaa ya Shinyanga
Mkutano wa hadhara ukiendelea katika kata ya Masekelo Manispaa ya Shinyanga.

Picha zote na Kadama Malunde - Malunde 1 blog


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com
Previous Post Next Post