Shirika lisilo la Kiserikali Perfomance Woman kwa kushirikiana na Shirika la Theatre Arts Feminists wamefanya uraghibishi katika shule ya msingi Mugabe iliyopo kata ya Sinza wilaya ya Ubungo jijini Dar es salaam na kutoa elimu ya ukatili wa kijinsia kwa wanafunzi 720 kati yao wavulana ni 359 na wasichana ni 36.
Mkurugenzi wa Shirika la Theatre Arts Feminists, Aluwa Mkilindi na Mkurugenzi wa Shirika lisilo la Kiserikali Perfomance Woman, Rose Mwasubila wameelezea mazingira yanayopelekea ukatili na mbinu za kuepuka ukatili.
"Pia tumebaini changamoto zilizopo shuleni hapo za ukatili ikiwa ni pamoja na ubakaji na kupata visa mkasa vya ubakaji viwili na visa viwili vya ulawiti ambapo kesi zimeshughulikiwa kwa ushirikiano wa ofisi ya Mtendaji Kata.
Perfomance Woman na Theatre Arts Feminists tumefurahishwa na ushirikiano uliopo kati ya shule na uongozi wa ofisi ya kata hali inayopelekea matukio ya ukatili kupatiwa ufumbuzi kwa haraka",wamesema.
"Perfomance Woman na Theatre Arts Feminists (Taf group) tunaahidi kushikiana katika ujenzi wa nguvu za pamoja (TAPO) ili kuweza kufikia watu wengi zaidi na kuhakikisha tunapambana na ukatili wa kijinsia ndani ya jamii", wameeleza.
Mkurugenzi wa Shirika lisilo la Kiserikali Perfomance Woman, Rose Mwasubila akitoa elimu ya masuala ya ukatili wa kijinsia.

Mkurugenzi wa Shirika la Theatre Arts Feminists, Aluwa Mkilindi akitoa elimu ya kukomesha ukatili wa kijinsia
Mkurugenzi wa Shirika la Theatre Arts Feminists, Aluwa Mkilindi akitoa elimu ya kukomesha ukatili wa kijinsia
Social Plugin