Wanaharakati wa kutetea haki za wanawake na watoto kutoka Shirika lisilo la Kiserikali Perfomance Woman kwa kushirikiana na Shirika la Theatre Arts Feminists wameendelea na Kampeni ya kupambana na vitendo vya ukatili wa kijinsia katika shule mbalimbali jijini Dar es salaam.
Wanaharakati kutoka waingia shule kwa shule kupambana na ukatili walimu watoa rai wazazi kusimamia malezi ya watoto na kushirikiana na walimu ili kupambana na ukatili.
Wakizungumza wakati wa kutoa elimu ya masuala ya ukatili wa kijinsia katika shule za Msingi Uzuri na Sinza Jijini Dar es salaam wiki hii, Wanaharakati hao (Mkurugenzi wa Shirika la Theatre Arts Feminists, Aluwa Mkilindi na Mkurugenzi wa Shirika lisilo la Kiserikali Perfomance Woman, Rose Mwasubila) wametoa rai kwa walimu na wazazi kusimamia malezi ya watoto ili kulinda watoto dhidi ya ukatili wa kijinsia.
“Wiki hii tumefanikiwa kutoa elimu ya kukabiliana na ukatili wa kijinsia kwa wanafunzi 911 kati yao wavulana ni 467 na wasichana 444 katika shule ya msingi Uzuri na wanafunzi 610 wasichana 320 na wavulana 290 katika shule ya msingi Sinza. Tumefurahishwa na uongozi wa dawati la jinsia katika shule ya Uzuri inayoongozwa na mwalimu wa malezi Rehema Issa Idd ambaye ameelezea faida za uwepo wa dawati hilo na kuomba wadau kuendelea kushirikiana ili kupamabana na ukatili wa kijinsia ndani ya jamii”,wameeleza Wanaharakati hao.
“Perfomance Woman na Theatre Arts Feminists (Taf group) tunaahidi kushikiana katika ujenzi wa nguvu za pamoja (TAPO) ili kuweza kufikia watu wengi zaidi na kuhakikisha tunapambana na ukatili wa kijinsia ndani ya jamii. Tunaiomba jamii kutoa ushirikiano na kuimarisha malezi ya watoto kwani kumekuwa na vitendo vya ukatili wamekuwa wakifanyiwa watoto”,wameongeza.
Shirika lisilo la Kiserikali Perfomance Woman kwa kushirikiana na Shirika la Theatre Arts Feminists pia limefanya uraghibishi katika shule ya msingi Mugabe iliyopo kata ya Sinza wilaya ya Ubungo jijini Dar es salaam na kutoa elimu ya ukatili wa kijinsia kwa wanafunzi 720 kati yao wavulana ni 359 na wasichana ni 36.
Mkurugenzi wa Shirika la Theatre Arts Feminists, Aluwa Mkilindi akitoa elimu ya kukomesha ukatili wa kijinsia katika shule ya Msingi Uzuri jijini Dar es salaam

Mkurugenzi wa Shirika lisilo la Kiserikali Perfomance Woman, Rose Mwasubila akitoa elimu ya kukomesha ukatili wa kijinsia katika shule ya Msingi Uzuri jijini Dar es salaam

Mkurugenzi wa Shirika la Theatre Arts Feminists, Aluwa Mkilindi akitoa elimu ya kukomesha ukatili wa kijinsia katika shule ya Msingi Sinza jijini Dar es salaam

Mkurugenzi wa Shirika lisilo la Kiserikali Perfomance Woman, Rose Mwasubila akitoa elimu ya kukomesha ukatili wa kijinsia katika shule ya Msingi Sinza jijini Dar es salaam