Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Mhe. Joseph Modest Mkude akizungumza kwenye kikao cha Tathmini ya utekelezaji wa miradi ya kusambaza umeme vijijini mkoani Shinyanga.
Na Mwandishi Wetu - Shinyanga
Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Mhe. Joseph Modest Mkude ametoa muda wa mwezi mmoja na nusu kwa wakandarasi wanaotekeleza Mradi wa Kusambaza umeme vijijini kukamilisha kazi waliyopewa na Serikali ili wananchi waanze kunufaika na huduma ya nishati ya umeme.
Mhe. Mkude ambaye ni Mkuu wa wilya ya Kishapu ametoa agizo hilo leo Jumatatu Januari 30,2023 kwenye kikao cha Tathmini ya utekelezaji wa miradi ya kusambaza umeme vijijini kilichofanyika katika ofisi za Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga.
Mkude amewataka wakandarasi hao kuwasilisha ripoti ya utekelezaji wa miradi hiyo kila wiki kwa wakuu wa wilaya zote na Ofisi ya Mkuu Mkoa.
"Utekelezaji wa miradi unasuasua sana na mkoa hauridhishwi na kasi yenu, endapo hamtajirekebisha Serikali haitasita kusitisha mikataba yenu", amesisitiza.
Naye Mkurugenzi wa Uendelezaji wa Masoko na Teknolojia wa Wakala wa Nishati Vijijini (Rural Energy Agency – REA)Mhandisi Advera Mwijage amesema hakutakuwa na muda wa nyongeza kwa wakandarasi na kuwataka wazingatie mikataba yao.
Mhandisi Mwijage amewataka wakandarasi kushirikisha viongozi wa ngazi zote kuanzia vijiji, wilaya na mikoa pamoja na wananchi wakati wa utekelezaji wa mradi ili kuweza kuondoa changamoto za malalamiko ya wananchi.
Kwa upande wao, Wakandarasi wanaotekeleza mradi huo, wameahidi kurekebisha kasoro zilizojitokeza na kuahidi kukamilisha miradi kwa mujibu wa mikataba waliyoingia na Serikali.
Mkurugenzi wa SUMA JKT Electric Co. Ltd ambao wanatekeleza Mradi katika wilaya ya Shinyanga Kishapu, Meja Simon Mhame amesema wameongeza vibarua na wameshaagiza vifaa vya kutosha kukamikisha Mradi hivyo watatimiza na kutii maagizo ya Serikali.
Mkurugenzi Mtendani wa Kampuni ya Ukandarasi ya Tontan Project Technology Co. Ltd, bw. Zheng Pengtao wanaotekeleza mradi wa umeme wilayani Kahama amesema watahakikisha wanakamilisha usambazaji wa umeme kwa wakati katika vijiji vyote kwa mujibu wa mkataba waliosaini na serikali.
Mradi wa Kusambaza Umeme Vijijini Awamu ya Tatu Mzunguko wa Pili utanufaisha vijiji 216 mkoani Shinyanga kwa gharama ya zaidi ya shilingi Bilioni 56 ambapo Wakandarasi wanaosimamia mradi wa usambazaji umeme wilayani Kahama, Shinyanga na Kishapu kuwa ni Suma JKT na Tontan Project Technology Co. Ltd.
Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Mhe. Joseph Modest Mkude akizungumza kwenye kikao cha Tathmini ya utekelezaji wa miradi ya kusambaza umeme vijijini mkoani Shinyanga. Picha na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Mhe. Joseph Modest Mkude akizungumza kwenye kikao cha Tathmini ya utekelezaji wa miradi ya kusambaza umeme vijijini mkoani Shinyanga
Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Mhe. Joseph Modest Mkude akizungumza kwenye kikao cha Tathmini ya utekelezaji wa miradi ya kusambaza umeme vijijini mkoani Shinyanga
Mkurugenzi wa Uendelezaji wa Masoko na Teknolojia wa Wakala wa Nishati Vijijini (REA) Mhandisi Advera Mwijage akizungumza kwenye kikao cha Tathmini ya utekelezaji wa miradi ya kusambaza umeme vijijini mkoani Shinyanga

Mkurugenzi wa Uendelezaji wa Masoko na Teknolojia wa Wakala wa Nishati Vijijini (REA) Mhandisi Advera Mwijage (wa pili kushoto) akizungumza kwenye kikao cha Tathmini ya utekelezaji wa miradi ya kusambaza umeme vijijini mkoani Shinyanga

Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Mhe. Joseph Modest Mkude akiwa kwenye kikao cha Tathmini ya utekelezaji wa miradi ya kusambaza umeme vijijini mkoani Shinyanga
Mkurugenzi wa SUMA JKT Electric Co. Ltd , Meja Simon Mhame akizungumza kwenye kikao cha Tathmini ya utekelezaji wa miradi ya kusambaza umeme vijijini mkoani Shinyanga
Mkurugenzi Mtendani wa Kampuni ya Ukandarasi ya Tontan Project Technology Co. Ltd, bw. Zheng Pengtao akielezea jitihada wanazofanya kuhakikisha wanakamilisha usambazaji wa umeme kwa wakati kwenye vijiji kwa mujibu wa mkataba waliosaini na serikali.
Wadau wakiwa kwenye kikao cha Tathmini ya utekelezaji wa miradi ya kusambaza umeme vijijini mkoani Shinyanga
Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Mhe. Joseph Modest Mkude akizungumza kwenye kikao cha Tathmini ya utekelezaji wa miradi ya kusambaza umeme vijijini mkoani Shinyanga.
Picha na Kadama Malunde - Malunde 1 blog