POLISI SHINYANGA WAPANDA MITI KAMBINI, HOSPITALI MPYA YA RUFAA.... DC MBONEKO ASISITIZA "MARUFUKU KUKATA MITI OVYO, ILINDWE NA IKUE"



Kamanda wa Jeshi la Polisi mkoani Shinyanga Janeth Magomi (kushoto) akiwa na Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko wakipanda miti.

Na Marco Maduhu, SHINYANGA

JESHI la Polisi mkoani Shinyanga, limepanda miti katika Hospitali ya Rufaa mkoa wa Shinyanga iliyopo Mwawaza na Kambi ya Jeshi hilo, ili kuboresha mazingira pamoja na kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi.

Zoezi hilo la upandaji miti limefanyika leo Januari 13, 2023 na kupandwa miti 1000, ambapo katika kambi ya Jeshi la Polisi (FFU) imepandwa miti 200 na Hospitali ya Rufaa imepandwa miti 800 ya matunda na kivuli.

Akizungumza wakati wa kupanda miti, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga ACP Janeth Magomi amesema Jeshi hilo linaunga mkono juhudi za Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, katika kampeni ya upandaji miti ili kuboresha mazingira na kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi.

“Jeshi la Polisi mkoani Shinyanga tumepanda Miti 1000, ambapo Miti 800 tumepanda hapa katika hospitali ya Rufaa ya Mkoa, na Miti 200 tumeipanda kambini, lengo ni kuunga mkono juhudi za viongozi wetu katika kampeni ya upandaji miti kuboresha mazingira na kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi,”amesema Magomi.

Naye Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko, amepongeza Jeshi la Polisi kwa upandaji miti, huku akipiga marufuku ukataji wa miti hovyo bila ya kuwa na vibali, pamoja na wafugaji kupitisha mifugo yao kwenye miti na kuiharibu.

“Katika kampeni ya upandaji miti tunataka Shinyanga iwe ya kijani, na miti ambayo tunaipanda tunataka ilindwe na ikue, na tunatekeleza maagizo ya Makamu wa Rais ya kupanda Miti milioni 1.5 kila mwaka na Shinyanga tunakwenda vizuri,”amesema Mboneko.

Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Rufaa mkoa wa Shinyanga Dk. Luzila John, amesema hospitali hiyo ni mpya ambayo ipo Mwawaza na kushukuru upandaji huo wa miti ili kuboresha mazingira na kuahidi kuitunza miti hiyo.

Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko akizungumza kwenye zoezi la upandaji miti.

Kamanda wa Jeshi la Polisi mkoani Shinyanga Janeth Magomi akizungumza kwenye zoezi la upandaji miti.

Afisa Mazingira na Maliasili Manispaa ya Shinyanga Ezra Manjerenga akizungumza kwenye zoezi hilo la upandaji miti.

Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko akipanda mti.

Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko akipanda mti.

Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Rufaa mkoani Shinyanga Dk. Luzila John akipanda mti.

Kamanda wa Jeshi la Polisi mkoani Shinyanga Janeth Magomi akipanda mti.

Zoezi la upandaji miti likiendelea.

Zoezi la upandaji miti likiendelea.
Zoezi la upandaji miti likiendelea.

Zoezi la upandaji miti likiendelea.

Zoezi la upandaji miti likiendelea.

Zoezi la upandaji miti likiendelea.

Askari Polisi wakiwa wameshika miche ya miti kwa ajili ya kuipanda.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com
Previous Post Next Post