Afisa uhifadhi wa wanyamapori daraja la kwanza wa hifadhi ya Taifa ya Serengeti, Deus Mwakajegele ameuawa kwa kuchomwa mshale na watu wasiojulikana alipokuwa akitekeleza majukumu yake ya kulinda hifadhi ya Serengeti Mkoani Mara.
Tukio hilo limetokea jana Jumamosi Januari 21, 2023 katika eneo la Nyanungu wilayani Tarime baada ya kuchomwa mshale wenye sumu kichwani na kufariki katika hospitali ya Seliani Arusha alipopelekwa kwa ajili ya matibabu.
Mkuu wa Mkoa wa Mara, Meja Jenerali Suleiman Mzee amesema kuwa tukio hilo limetokea katika eneo lililokuwa na mgogoro ambao ulikuwa umetolewa maamuzi na vyombo vya dola.
Social Plugin