Mwalimu akimchapa mwanafunzi
Waziri wa Elimu Prof. Adolf Mkenda amesema kuwa Mwalimu anayeonekana kwenye video fupi inayosambaa mitandaoni akimchapa mwanafunzi kwenye nyayo za miguu yake huku amemkanyaga tayari amekwishachukuliwa hatua za kusimamishwa kazi.
Kwa mujibu wa Waziri wa Maendeleo ya Jamii Dkt. Dorothy Gwajima, amesema Mwalimu huyo ni wa shule ya msingi iliyopo wilayani Kyerwa mkoani Kagera na tukio hilo limetokea Januari 10, 2023.
Aidha waziri Dkt Gwajima akatoa rai kwa Walimu, "Waalimu zingatieni utaratibu wa adhabu kwa wanafunzi, lazima sheria ziheshimiwe,".
Social Plugin