Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

MIGODI YA BARRICK YAWEKA REKODI YA UZALISHAJI NA KUPATA THAMANI YA MUDA MREFU

Rais na Afisa Mtendaji Mkuu wa Barrick, Mark Bristow akizungumza na Waandishi wa habari katika Mgodi wa Bulyanhulu. Kushoto ni Meneja wa Barrick Tanzania, Melkiory Ngido, kulia ni Naibu Waziri wa Madin Dkt. Steven Kiruswa.

Na Kadama Malunde - Malunde 1 blog

 Kampuni ya Dhahabu ya Barrick  inayomiliki Migodi miwili ya North Mara na Bulyanhulu imeongeza pato lake kwa pamoja hadi kufikia wakia 547,000 kwa mwaka 2022, na kufanikisha hatua nyingine ya kuelekea hadhi ya Daraja la Kwanza.

Mgodi wa Dhahabu wa Daraja la Kwanza ni ule wenye hifadhi ya dhahabu yenye uwezo wa kuzalisha kwa angalau kipindi cha miaka 10, angalau wakia 500,000 za dhahabu kwa mwaka na jumla ya gharama za fedha taslimu kwa kila wakia kwa kipindi cha uhai wa mgodi ambazo ziko katika nusu ya chini ya grafu ya gharama za tasnia husika.

Akitoa taarifa kwa vyombo vya habari na wadau wengine katika Mgodi wa Bulyanhulu Januari 25,2023 , Rais na Afisa Mtendaji Mkuu wa Barrick, Mark Bristow, amesema tangu kampuni ichukue jukumu la udhibiti wa migodi hiyo mwaka 2019 imefanikiwa kufanya mageuzi makubwa katika shughuli zilizokuwa zimekufa au zikielekea kufa na kuwa mali zenye thamani ya hali ya juu kwa utendaji wake kwa sasa, matarajio yake ya baadaye, na kukubalika kwake katika jamii.

Aidha amesema utafutaji wa madini unaendelea kutoa fursa za kuongeza ukubwa wa akiba ya miamba yenye madini katika migodi yote miwili huku akieleza kuwa kipindi cha mpito cha mgodi wa North Mara kuelekea uchimbaji wa mmiliki unafanikiwa kwa kuongeza kwa kasi upanuzi wake unaoendelea wa chimbo la wazi kukiwa na uboreshaji wa ufanisi na gharama, wakati maendeleo ya kiteknolojia katika shughuli za uchimbaji wa chini kwa chini yanaongeza tija. 

Ameongeza kuwa Mipango ya kuanzisha upya uchimbaji katika chimbo la Gena inaendelea vizuri.

Katika mgodi wa Bulyanhulu, amesema shabaha kuu ni kuharakisha maendeleo ili kuukabili upungufu wake kwa kuifikia akiba mpya ya madini katika upande wa magharibi na upatikanaji wa wake.

"Leo hii, migodi hiyo inatambuliwa na serikali na jamii kama biashara zinazowajibika kwa jamii kwa kutengeneza fursa zenye manufaa makubwa na kuzishirikisha jamii na wadau wote katika fursa hizo na katika manufaa yenyewe, na kama mbia mkuu katika maendeleo ya kijamii na kiuchumi nchini Tanzania," alisema.

"Mwaka jana, North Mara ilitambuliwa rasmi kama mlipakodi mkubwa zaidi wa Tanzania na Bulyanhulu ilitunukiwa tuzo ya Mwajiri Bora Anazingatia Masharti na Matakwa ya Sheria, iliyotolewa na Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii. North Mara na Bulyanhulu pia zilipokea tuzo za mshindi wa kwanza na wa pili mtawalia za kutambua mchango wao kwa Uuzaji wa Madini nje ya nchi na kwa uzalishaji wa fedha za kigeni.

Migodi yote miwili imetoka safari ya mbali sana na tunatarajia kuendelea na safari hiyo kupitia ubia wetu wa Twiga na serikali”, alisema Bristow

Alisema tangu ichukue jukumu la udhibiti mnamo mwaka 2019, Barrick imeingiza dola za kimarekani bilioni 2.4 katika uchumi wa Tanzania. Mwaka jana, ililipa dola za kimarekani milioni 303 za kodi, mrabaha, ushuru, gawio na ulipaji wa mikopo ya wanahisa na dola za kimarekani milioni 476 kwa wasambazaji na watoaji wa huduma wa ndani .

"Kadiri migodi ilivyoendelea kukua, imeendelea kuweka kipaumbele cha utoaji wa ajira kwa watu wa ndani. Nguvu kazi yake hivi sasa tayari ina Watanzania wapatao 96%, huku 45% ya waajiriwa wapya wakitoka katika jamii zinazoizunguka migodi. Kupitia kamati zake za maendeleo ya jamii, migodi hiyo imewekeza zaidi ya dola za kimarekani milioni 10 katika miradi ya kuboresha huduma za afya, elimu, upatikanaji wa maji ya bomba na miundombinu ya barabara",alieleza.

Kwa upande wake, Naibu Waziri wa Madin Dkt. Steven Kiruswa ameishukuru Barrick na Kampuni tanzu ya Twiga kwa mafanikio makubwa yanayozidi kuonekana kupitia uwekezaji hapa nchini.

“Tuendelee kupiga vita utoroshaji madini, tuendelee kuwapa ushirikiano kampuni ya Barrick ili uwekezaji uwe na tija kwa wananchi. Tunataka kampuni ziwape kipaumbele wazawa ambapo tunashukuru Barrick imeajiri watanzania asilimia 96%”,alisema Dkt. Kiruswa.

Naye Mbunge wa Jimbo la Msalala Mhe. Idd Kassim amesema uhusiano uliopo kati ya Mgodi wa Bulyanhulu na jamii ni mzuri ambapo fedha zinazotolewa na mgodi zinaleta tija kwa jamii.

Mkuu wa Mkoa wa Geita Martine Shigela na Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Dkt. Yahaya Nawanda wamesema wataendelea kushirikiana na Kampuni ya Barrick na kuhakikisha fedha zinazotolewa zinainufaisha jamii.
Naibu Waziri wa Madin Dkt. Steven Kiruswa akizungumza na waandishi wa habari

Rais na Afisa Mtendaji Mkuu wa Barrick, Mark Bristow akiteta na Naibu Waziri wa Madin Dkt. Steven Kiruswa (kulia).
Rais na Afisa Mtendaji Mkuu wa Barrick, Mark Bristow akizungumza na Waandishi wa habari katika Mgodi wa Bulyanhulu. Kushoto ni Meneja wa Barrick Tanzania, Melkiory Ngido, kulia ni Naibu Waziri wa Madin Dkt. Steven Kiruswa.
Rais na Afisa Mtendaji Mkuu wa Barrick, Mark Bristow akizungumza na Waandishi wa habari katika Mgodi wa Bulyanhulu. Kushoto ni Meneja wa Barrick Tanzania, Melkiory Ngido, kulia ni Naibu Waziri wa Madin Dkt. Steven Kiruswa.
Rais na Afisa Mtendaji Mkuu wa Barrick, Mark Bristow akizungumza na Waandishi wa habari katika Mgodi wa Bulyanhulu.

Meneja wa Barrick Tanzania, Melkiory Ngido akizungumza na waandishi wa habari

Meneja wa Barrick Tanzania, Melkiory Ngido akizungumza na waandishi wa habari
 Mbunge wa Jimbo la Msalala Mhe. Idd Kassim akizungumza
Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Dkt. Yahaya Nawanda akizungumza 
Mkuu wa Mkoa wa Geita Martine Shigela akizungumza
Wadau wakiwa ukumbini
Wafanyakazi wa Barrick wakiwa ukumbini
Wafanyakazi wa Barrick wakiwa ukumbini
Viongozi  wa mikoa ya Geita na Shinyanga wakiwa ukumbini
Wafanyakazi wa Barrick na wadau wakiwa ukumbini
Wafanyakazi wa Barrick na wadau wakiwa ukumbini
Wafanyakazi wa Barrick wakiwa ukumbini.

Picha zote na Kadama Malunde - Malunde 1 blog

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com