Mwenyekiti wa Kamati ya Hisani katika Jamii iliyoundwa na wadau wa Maendeleo katika Manispaa ya Shinyanga chini ya usimamizi wa Shirika la Thubutu Africa Initiatives bw. Joseph Ndatala (kulia) akimuonesha Katibu Tawala wilaya ya Shinyanga, Boniphace Chambi choo cha kisasa cha wasichana katika shule ya msingi Lubaga Manispaa ya Shinyanga.
Na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Kamati ya Hisani katika Jamii (Community Philanthropy) iliyoundwa na wadau wa Maendeleo katika Manispaa ya Shinyanga chini ya usimamizi wa Shirika lisilokuwa la Kiserikali la Thubutu Africa Initiatives imekabidhi Choo cha Kisasa cha Wasichana Shule ya Msingi Lubaga ili kutatua changamoto ya choo kwa wanafunzi wa kike.
Hafla fupi ya makabidhiano imefanyika katika shule ya Msingi Lubaga yenye jumla ya wanafunzi 605 ( wasichana 308 , wavulana 297) iliyopo katika Manispaa ya Shinyanga leo Alhamisi Januari 26,2023 ambapo Mgeni rasmi alikuwa Katibu Tawala Wilaya ya Shinyanga Boniphace Chambi.
Akizungumza wakati wa hafla hiyo, Chambi amelipongeza Shirika la Thubutu Africa Initiatives kwa kuanzisha wazo la Hisani ya Jamii kwa ajili ya kujenga choo cha kisasa katika shule hiyo.
“Tunawashukuru sana Thubutu Africa Initiatives kwa kuja na wazo hili zuri, lakini pia wadau na wananchi wote mliojitokeza kufanikisha ujenzi wa choo hiki cha kisasa”,amesema Chambi.
“Ninakipokea choo hiki cha kisasa kilichojengwa kwa hisani ya jamii, kitaanza kufanya kazi siku ya Jumatatu. Hii inaonesha dhahiri kwamba kumbe siyo lazima tusubiri wafadhili waje kutusaidia, lazima tuchukue hatua kwanza sisi wenyewe”,ameongeza Chambi.
Akizungumza wakati wa makabidhiano hayo, Mkurugenzi wa Shirika la Thubutu Africa Initiatives (TAI), Jonathan Kifunda Manyama amesema ujenzi wa choo hicho uliochukua miezi mitano unatokana na mafunzo yaliyotolewa na shirika hilo kwa wadau kuhusu namna mradi wa hisani katika jamii unavyotekelezwa.
“Tarehe 20/05/2022 Shirika letu la Thubutu Africa Initiatives lilizindua mradi wa hisani katika jamii katika ukumbi wa Vigmark hotel ambapo wajumbe mbalimbali kutoka serikalini pamoja na mashirika yasiyo ya kiserikali walihudhuria. Baada ya mafunzo hayo kati ya kata nne zilizokuwa na wajumbe walioziwakilisha kata moja (Lubaga) ilichaguliwa ili kutekelezwa mradi wa hisani katika jamii kwa vitendo ili kutatua changamoto ya choo kwa watoto wa kike ambapo kata tatu zilizobaki( Mjini, Mwamalili na Old-Shinyanga zilitumika kufanyiwa utafiti wa hojaji kuhusu uelewa na utayari wa wanajamii katika kuchangia maendeleo yao wenyewe”,amesema Kifunda.
Mkurugenzi huyo wa Thubutu Africa Initiaves ametumia fursa hiyo kuwashukuru wadau na wananchi walioshiriki kwa hali na mali kufanikisha kukamilika kwa ujenzi wa choo cha wasichana katika shule ya Msingi Lubaga.
Akitoa taarifa ya ujenzi, Mwenyekiti wa Kamati ya Hisani, Joseph Ndatala amesema ujenzi wa choo hicho ulianza Julai 7,2022 na kukamilika Desemba 12,2022 ambapo zoezi la ukusanyaji rasmali na utoaji elimu lilikuwa endelevu tangu siku ya kwanza hadi tarehe ya mwisho lilikuwa likiendelea kwa sababu mahitaji hayakukusanywa kwa wakati mmoja na kukamilika.
“Kwa mujibu wa Mchoro wa ujenzi na makadirio ya bajeti (BOQ) ujenzi wa choo cha Wasichana Lubaga ulikadiriwa kutumia kiasi cha Milioni 23 (Tsh 23,397,984) hata hivyo ujenzi huu umetumia kiasi cha Shilingi Milioni 11 (Tsh 11,063,800/=) ikiwa ni pamoja na nguvu kazi . Pamoja na bajeti hii kuwa chini tofauti na makadirio ya awali bado kiwango cha ubora wa choo umebaki kuwa ni uleule, hii inatokana na kwamba tumetumia mafundi wa kawaida kutoka kwenye jamii yetu (Local fundi) na ujitoleaji wa jamii ambao umepunguza gharama nyingine ambazo zingeongeza bajeti”,ameeleza Ndatala.
“Kamati ya Hisani imefanikiwa kukamilisha ujenzi wa matundu sita ya choo cha wasichana Lubaga pamoja na chumba maalumu cha wasichana kwa ajili ya kujistiri. Hivyo, wasichana watasoma kwa utulivu na mahudhurio yao katika vipindi darasani kuongezeka na kuendeleza kiwango cha ufaulu kuwa juu na ubora wa elimu wanayoipata. Mafanikio haya hayakuwa mepesi kwa sababu miradi ya aina hii haijazoeleka katika maeno yetu na Tanzania hususani Manispaa ya Shinyanga. Hata hivyo umahiri na uvumilivu wa wajumbe wa Kamati umekuwa chanzo kikuu cha mafanikio ya kazi hii ya ujenzi wa choo hiki”,ameongeza Ndatala.
Katika hatua nyingine Ndatala amesema Kamati ya hisani katika utekelezaji wa mradi huo imebaini kuwa upo uwezekano mkubwa wajamii kushiriki katika shughuli za maendeleo katika kusaidia jamii yao wao wenyewe, hivyo wanapendekeza mradi huo utekelezwe mahali pengine katika Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga.
“Kwa kuwa mradi huu umekamilika kwa kiwango cha juu lakini hakuna miundo mbinu ya maji ndani ya choo, Kamati inaomba hadhira hii kufanikisha kuchangisha kiasi cha Tsh 400,000/= kwa ajili ya kuweka maji ndani ya choo hiki. Kamati pia inaomba wadau kuchangia ukarabati wa choo cha wavulana katika shule hii kwani kimechakaa hali ambayo inawafanya wanafunzi wa kiume kujisikia wanyonge ukilinganisha na choo cha kisasa tulichokamilisha ujenzi wake ambacho ni cha wasichana”, amesema.
Nao baadhi ya wanafunzi wameshukuru kujengwa kwa choo hicho wakisema kitawaondolea adha ya kupanga foleni wakati wa kujisaidia lakini pia kujiepusha na magonjwa huku wanafunzi wa kiume wakiomba choo chao kifanyiwe ukarabati au wajengewe choo kipya.
Mwenyekiti wa Kamati ya Hisani katika Jamii (Community Philanthropy) iliyoundwa na wadau wa Maendeleo katika Manispaa ya Shinyanga chini ya usimamizi wa Shirika la Thubutu Africa Initiatives bw. Joseph Ndatala (kulia) akimuonesha Katibu Tawala wilaya ya Shinyanga, Boniphace Chambi choo cha kisasa cha wasichana katika shule ya msingi Lubaga Manispaa ya Shinyanga leo Alhamisi Januari 26,2023. Picha na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Katibu Tawala wilaya ya Shinyanga, Boniphace Chambi akiangalia chumba cha usiri kwa wanafunzi wa kike kilichopo kwenye choo cha kisasa cha wasichana katika shule ya msingi Lubaga Manispaa ya Shinyanga
Mwenyekiti wa Kamati ya Hisani katika Jamii iliyoundwa na wadau wa Maendeleo katika Manispaa ya Shinyanga chini ya usimamizi wa Shirika la Thubutu Africa Initiatives bw. Joseph Ndatala akimwelezea Katibu Tawala wilaya ya Shinyanga, Boniphace Chambi kuhusu ujenzi wa choo cha kisasa cha wasichana katika shule ya msingi Lubaga Manispaa ya Shinyanga
Mwenyekiti wa Kamati ya Hisani katika Jamii iliyoundwa na wadau wa Maendeleo katika Manispaa ya Shinyanga chini ya usimamizi wa Shirika la Thubutu Africa Initiatives bw. Joseph Ndatala akimwelezea Katibu Tawala wilaya ya Shinyanga, Boniphace Chambi kuhusu ujenzi wa choo cha kisasa cha wasichana katika shule ya msingi Lubaga Manispaa ya Shinyanga
Mwenyekiti wa Kamati ya Hisani katika Jamii iliyoundwa na wadau wa Maendeleo katika Manispaa ya Shinyanga chini ya usimamizi wa Shirika la Thubutu Africa Initiatives bw. Joseph Ndatala (wa pili kulia), Katibu Tawala wilaya ya Shinyanga, Boniphace Chambi na viongozi mbalimbali wakiondoka katika choo cha kisasa cha wasichana katika shule ya msingi Lubaga Manispaa ya Shinyanga
Mwenyekiti wa Kamati ya Hisani katika Jamii iliyoundwa na wadau wa Maendeleo katika Manispaa ya Shinyanga chini ya usimamizi wa Shirika la Thubutu Africa Initiatives bw. Joseph Ndatala (wa pili kulia), Katibu Tawala wilaya ya Shinyanga, Boniphace Chambi na viongozi mbalimbali wakiondoka katika choo cha kisasa cha wasichana katika shule ya msingi Lubaga
Muonekano wa choo cha kisasa cha wasichana katika shule ya msingi Lubaga Manispaa ya Shinyanga
Katibu Tawala wilaya ya Shinyanga, Boniphace Chambi akizungumza wakati wa makabidhiano ya choo cha kisasa cha wasichana katika shule ya msingi Lubaga Manispaa ya Shinyanga
Katibu Tawala wilaya ya Shinyanga, Boniphace Chambi akizungumza wakati wa makabidhiano ya choo cha kisasa cha wasichana katika shule ya msingi Lubaga Manispaa ya Shinyanga
Mkurugenzi wa Shirika la Thubutu Africa Initiatives (TAI), Jonathan Kifunda Manyama akizungumza wakati wa makabidhiano ya choo cha kisasa cha wasichana katika shule ya msingi Lubaga Manispaa ya Shinyanga
Mwenyekiti wa Kamati ya Hisani katika Jamii iliyoundwa na wadau wa Maendeleo katika Manispaa ya Shinyanga chini ya usimamizi wa Shirika la Thubutu Africa Initiatives bw. Joseph Ndatala akitoa taarifa ya ujenzi wa choo cha kisasa katika shule ya msingi Lubaga Manispaa ya Shinyanga.
Mwenyekiti wa Kamati ya Hisani katika Jamii iliyoundwa na wadau wa Maendeleo katika Manispaa ya Shinyanga chini ya usimamizi wa Shirika la Thubutu Africa Initiatives bw. Joseph Ndatala akitoa taarifa ya ujenzi wa choo cha kisasa katika shule ya msingi Lubaga Manispaa ya Shinyanga.
Naibu Meya wa Manispaa ya Shinyanga, Esther Makune akizungumza wakati wa makabidhiano ya choo cha kisasa cha wasichana katika shule ya msingi Lubaga Manispaa ya Shinyanga
Mwanafunzi wa shule ya Msingi Lubaga akitoa neno la shukrani wakati wa makabidhiano ya choo cha kisasa cha wasichana katika shule ya msingi Lubaga Manispaa ya Shinyanga
Mwakilishi wa Mashirika yasiyo ya kiserikali John Shija kutoka PACESH akizungumza wakati wa makabidhiano ya choo cha kisasa cha wasichana katika shule ya msingi Lubaga Manispaa ya Shinyanga
Diwani wa kata ya Lubaga Reuben Dotto akizungumza wakati wa makabidhiano ya choo cha kisasa cha wasichana katika shule ya msingi Lubaga Manispaa ya Shinyanga
Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Shinyanga Mjini, Anord Makombe akizungumza wakati wa makabidhiano ya choo cha kisasa cha wasichana katika shule ya msingi Lubaga Manispaa ya Shinyanga
Wanafunzi wakifuatilia hafla ya makabidhiano ya choo cha kisasa cha wasichana katika shule ya msingi Lubaga Manispaa ya Shinyanga
Mzazi akielezea namna alivyoshiriki katika ujenzi wa choo cha kisasa cha wasichana katika shule ya msingi Lubaga Manispaa ya Shinyanga
Wadau mbalimbali wakiwa kwenye hafla ya makabidhiano ya choo cha kisasa cha wasichana katika shule ya msingi Lubaga Manispaa ya Shinyanga
Wadau mbalimbali wakiwa kwenye hafla ya makabidhiano ya choo cha kisasa cha wasichana katika shule ya msingi Lubaga Manispaa ya Shinyanga
Wadau mbalimbali wakiwa kwenye hafla ya makabidhiano ya choo cha kisasa cha wasichana katika shule ya msingi Lubaga Manispaa ya Shinyanga
Wadau mbalimbali wakiwa kwenye hafla ya makabidhiano ya choo cha kisasa cha wasichana katika shule ya msingi Lubaga Manispaa ya Shinyanga
Katibu Tawala wilaya ya Shinyanga, Boniphace Chambi, wadau na Kamati ya Hisani katika Jamii iliyofanikisha ujenzi wa choo cha wasichana katika shule ya msingi Lubaga wakipiga picha ya kumbukumbu.
Katibu Tawala wilaya ya Shinyanga, Boniphace Chambi, wadau wakipiga picha ya kumbukumbu.
Katibu Tawala wilaya ya Shinyanga, Boniphace Chambi, wadau, mwakilishi wa Mbunge wa Jimbo la Shinyanga Mjini, Madiwani wakipiga picha ya kumbukumbu.
Katibu Tawala wilaya ya Shinyanga, Boniphace Chambi, wadau na wanafunzi wa shule ya msingi Lubaga wakipiga picha ya kumbukumbu.
Katibu Tawala wilaya ya Shinyanga, Boniphace Chambi, wadau na wanafunzi wa shule ya msingi Lubaga wakipiga picha ya kumbukumbu.
Picha na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Social Plugin