Na Abel Paul wa Jeshi la Polisi
Wakazi wa wilaya ya Longido Mkoani Arusha wamepongezwa kwa ujenzi wa kituo kidogo cha Polisi Mundalala wenye ramani ya kisasa ambayo imezingatia haki za binadamu.
Kauli hiyo imetolewa leo Januari 15 na Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Jumanne Sagini wakati akikagua maendeleo ya ujenzi wa kituo hicho kinachojengwa na nguvu ya wananchi.
Mheshimiwa Sagini amesema kuwa wizara yake imefurahishwa sana na kitendo cha wananchi kujitoa katika masuala ya kiusalama ambapo amewaomba wananchi wengine kuendelea kujitoa katika kazi za kiusalama ili kukomeasha uhalifu katika Nchi.
Aidha amempongeza Naibu Waziri wa Madini Dkt. Steven Kiruswa kwa kutoa ahadi ya mifuko ya saruji. Ili kufanikisha ujenzi huo ambapo amesema wao kama wizara wanakwenda kuket pamoja na Mkuu wa Jeshi la Polisi ili waweka miakakati ya haraka kukamilisha.
Naye Naibu Waziri wa Madini Dkt. Steven Kiruswa amemshukuru naibu waziri huyo kwa kufika katika wilaya kijiji cha Mundalala ambapo amehaidi kutoa mifuko ya saruji mia moja.
Nao baadhi ya wananchi walioshiriki katika ujenzi wa kituo hicho wameiomba serkali hususani wizara ya mambo ya ndani ya Nchi kuwachangia ili kukamilisha ujenzi huo
Akisoma taarifa ya ujenzi huo Mkuu wa Polisi wilaya ya Longido mrakibu wa Polisi SP REHA NCHEKI amesema zaidi ya milioni sabini na nane zinahitajika kukamilisha ujenzi huo.
Social Plugin