WIZARA YA UWEKEZAJI VIWANDA NA BIASHARA, YATOA MAFUNZO YA KAIZEN KWA WAMILIKI WA VIWANDA NA WATUMISHI WA SERIKALI


Mafunzo ya uhamasishaji falsafa ya KAIZEN yakitolewa kwa Wamiliki wa Viwanda Wafanyakazi na Watumishi wa Serikali

Na Marco Maduhu, SHINYANGA

WIZARA ya Uwekezaji, Viwanda na Biashara imetoa mafunzo ya uhamasishaji wa falsafa ya kupunguza gharama za uzalishaji kwenye viwanda, na kuongeza ufanisi wa utendaji kazi kwenye Ofisi za Serikali (KAIZEN).

Mafunzo hayo ambayo ni ya siku moja yametolewa leo Januari 26, 2023 katika ukumbi wa Mikutano wa Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga.

Mkuu wa Kitendo cha KAIZEN kutoka Wizara ya Uwekezaji, Viwanda na Biashara Richard Pweleza, akisoma hotuba kwa niaba ya Mkurugenzi wa Idara ya Viwanda kwenye mafunzo hayo, amesema Falsafa ya KAIZEN imechangia kukuza uchumi katika nchi ya Japan, na Tanzania ni miongoni mwa nchi 16 Barani Afrika ambazo zinatekeleza falsafa hiyo.

Amesema faida ya KAIZEN ni kuwezesha uongezaji endelevu wa ubora na tija wa bidhaa za viwandani, kupunguza muda wa utendaji kazi, gharama za uzalishaji, kuboresha usimamizi wa Rasilimali watu, fedha, na vitendea kazi.

“Neno KAIZEN linatokana na maeneno mawili ya KIJAPAN, KAI maana yake ni badiliko zuri na neon ZEN likiwa na maana ya maboresho endelevu, hivyo KAIZEN ni mabadiliko endelevu mazuri kuelekea kwenye ukuaji wa uchumi,”amesema Pweleza.

“Falsafa ya KAIZEN inahimiza ushirikishwaji, uwajibikaji kwenye taasisi, kampuni au kiwanda katika mlolongo mzima wa uzalishaji ili kuhimili ushindani, pia kuwepo na ubunifu katika kupunguza gharama zisizo za lazima viwandani ili kuongeza tija na ubora kwenye mnyororo wa thamani wa bidhaa na huduma,”ameongeza.

Naye Mgeni Rasmi Kaimu Katibu Tawala msaidizi sehemu ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji mkoani Shinyanga Dotto Maligisa, akisoma hotuba ya ufunguzi wa mafunzo hayo kwa niaba ya Katibu Tawala Mkoa wa Shinyanga, ameipongeza Serikali ya awamu ya sita kwa kuithamini sekta ya viwanda na kutambua mchango wake mkubwa na kuleta mafunzo hayo ya KAIZEN ili kuifikisha Tanzania kwenye uchumi wa kati ifikapo mwaka 2025.

“Nchi ya Japan haikujaliwa kuwa na rasilimali madini, misitu, mifugo, mafuta ya petrol, gesi asilia wala mazao ya kilimo, na Japani ni miongoni mwa nchi Nane zinazoitwa “G8” moja ya siri ya mafaniko ya Japan ni kuwekeza kwenye rasilimali watu na ubora wa bidhaa za viwandani,”amesema Maligisa.

Aidha, amewataka washiriki wa mafunzo hayo wakaitekeleze Falsafa hiyo ya KAIZEN kwa vitendo pamoja na kwenda kuwa mabalozi kwa wenzao na kujituma katika kazi, kuwa wabunifu na kuzingatia ubora wa bidhaa.

Baadhi ya washiriki wa mafunzo hayo wameipongeza Wizara ya Uwekezaji, Viwanda na Biashara kwa kuwapatia mafunzo hayo ya falsafa ya KAIZEN ambayo yamewajenga kiutendaji kazi.
Kaimu Katibu Tawala msaidizi sehemu ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji mkoani Shinyanga Dotto Maligisa, akisoma hotuba ya ufunguzi wa mafunzo hayo kwa niaba ya Katibu Tawala Mkoa wa Shinyanga.

Mkuu wa Kitendo cha KAIZEN kutoka Wizara ya Uwekezaji, Viwanda na Biashara Richard Pweleza, akizungumza kwenye mafunzo hayo.

Mwenyekiti wa Chemba ya Wafanyabishara wenye Viwanda na Kilimo (TCCIA), Mkoa wa Shinyanga Dk. Kulwa Meshack.

Meneja wa Shrika la kuhudumia Viwanda Vidogo (SIDO) Mkoa wa Shinyanga Hopeness Elia akizungumza kwenye mafunzo hayo.

Mkufunzi Mhandisi Emmanuel Zakayo akitoa mafunzo ya KAIZEN kwa washiriki.

Mkufunzi Juma Mantakara akitoa mafunzo ya KAIZEN kwa washiriki.

Washiriki wakifautilia mafunzo ya uhamasishaji wa Falsafa ya KAIZEN.

Washiriki wakiendelea na mafunzo.

Washiriki wakiendelea na mafunzo.

Washiriki wakiendelea na mafunzo.

Washiriki wakiendelea na mafunzo.

Washiriki wakiendelea na mafunzo.

Washiriki wakiendelea na mafunzo.

Washiriki wakiendelea na mafunzo.

Washiriki wakiendelea na mafunzo.

Washiriki wakiendelea na mafunzo.

Washiriki wakiendelea na mafunzo.

Washiriki wakiendelea na mafunzo.

Washiriki wakiendelea na mafunzo.

Washiriki wakiendelea na mafunzo.

Washiriki wakiendelea na mafunzo.

Washiriki wakiendelea na mafunzo.

Washiriki wakiendelea na mafunzo.

Washiriki wakiendelea na mafunzo.

Washiriki wakiendelea na mafunzo.

Washiriki wakiendelea na mafunzo.

Washiriki wakiendelea na mafunzo.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com
Previous Post Next Post