Mwanajeshi mmoja anauguza jeraha hospitalini baada ya kupigwa risasi mkononi na mwanaume anayeshukiwa kuwa jambazi kuwa kumuuliza kwa nini alikuwa akivuta bangi hadharani.
Timothy Mwangi alikuwa kwenye likizo katika kijiji chake cha Kihoni katika kaunti ya Murang'a kisa hicho kilipotokea Jumapili mchana.
Kwa mujibu wa Mwangi, alikuwa njiani akitembea kijijini kwao alipokutana na pikipiki iliyokuwa na mwendeshaji pamoja na abiria mmoja.
"Abira alikuwa anavuta bangi hali ambayo ilinifanya kumuuliza kwa nini alikuwa anavuta bangi hiyo," Mwangi amenukuliwa na gazeti la the Star.
Mwanajeshi huyo anasema kuwa mwendeshaji pikipiki alipunguza kasi, abiria huyo kushuka na kutembea hadi alipokuwa.
Abiria huyo alichomoa bastola na kuilekeza kwa mwanajeshi huyo ambaye aliinua mikono yake juu ishara ya kusalimu amri.
Mwangi anasimulia kuwa abiria huyo alichukua mkono wake wa kushoto kwa fujo na kumpiga risasi kwenye kiganja.
Risasi ilitokea upande wa pili na Mwangi kwenda chini kwa uchungu huku akibubujikwa na damu.
Kwa mujibu wa mwanajeshi huyo, wawili hao walirukia pikipiki yao na kuondoka eneo hilo bila kumwibia chochote.
Mwangi alikimbizwa katika Hospitali ya Kandara Level Four na baadate kuhamishiwa Thika Level Five ambako amelazwa, kwa mujibu wa polisi.
Hakuna mshukiwa aliyekamatwa kuhusiana na kisa hicho lakini juhusi za kulinasa genge hilo zinaendelea huku polisi wakiamini kuwa washukiwa walikuwa kwenye oparesheni ya ujambazi.
Chanzo - Tuko news
Social Plugin