Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

DKT MABULA ATAKA WANA CCM KUTUMIA FURSA YA MIKUTANO YA HADHARA KUJIBU HOJA

Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya Chama cha Mapinduzi ambaye ni Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula akivishwa Scarf mara baada ya kuwasili ofisi ya CCM mkoa wa Mwanza ilipofanyika sherehe ya kuwakaribisha wajumbe wa NEC Taifa tarehe 11 Januri 2023. Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya Chama cha Mapinduzi ambaye ni Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula akizungumza na wanachama wa CCM waliojitokeza katika sherehe za kuwakaribisha wajumbe wa NEC Taifa tarehe 11 Januari 2023 mkoani Mwanza. Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa Bi. Ellen Makungu Bogoje akizungumza kwenye sherehe za kuwakaribisha Wajumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa zilizofanyika ofisi ya CCM mkoa wa Mwanza tarehe 11 Januari 2023. Baadhi ya wana CCM waliojitokeza katika sherehe za kuwakaribisha wajumbe wa NEC Taifa ambao ni Dkt Angeline Mabula na Ellen Makungu Bogoje tarehe 11 Januari 2023. Vijana wa hamasa wa Chama cha Mapinduzi mkoa wa Mwanza wakifurahia wakati wa sherehe za kuwapokea wajumbe wa halmashauri Kuu ya CCM Taifa zilizofanyika ofisi ya CCM mkoa wa Mwanza tarehe 11 Januari 2023. Mkuu wa mkoa wa Mwanza Adam Malima akizungumza katika sherehe za kuwapokea wajumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa CCM zilizofanyika ofisi ya CCM mkoa wa Mwanza tarehe 11 Januari 2023.

**************************

Na Mwandishi Maalum, MWANZA

Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Chama cha Mapinduzi ambaye ni Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula amewataka wanachama wa Chama cha Mapinduzi nchini kutumia fursa ya kuruhusiwa mikutano ya hadhara kama njia ya kujibu hoja kwa kuelezea mafanikio ya yaliyofanywa na chama hicho.

Dkt Mabula amesema hayo tarehe 11 Januari 2023 katika ofisi ya Chama cha Mapinduzi mkoa wa Mwanza wakati wa mapokezi ya wajumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa waliochaguliwa hivi karibuni kwenye mkutano mkuu wa 10 wa CCM.

Amesema, wana CCM wasiangalie sasa ambapo mikutano imeruhusiwa na kuanza kubishana huku wakiacha kuangalia utekelezaji wa ilani ya Chama cha Mapinduzi na kuifanya kasuasua.

Kwa mujibu wa Dkt Mabula, Chama cha Mapinduzi kinayo matawi, Mashina pamoja na Kamati zake zake za siasa katika ngazi zote na kinachotakiwa ni kurudi kwa wanachama na kuhamasisha maendeleo huku wakikagua utekelezaji wa ilani ya CCM.

‘’Lazima kwenda kila ngazi kwa kukagua na kuangalia kama ilani inatekelezwa lakini siyo kwa kunyanyasa watumishi, hoja ya msingi hatutakiwi kuzifanya hoja zinazokuja kama kero za kujibishana na kila changamoto itakoyokuja igeuzwe kama fursa ya kusonga mbele.

Aidha, alimsifu na kumpongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Dkt Samia Suluhu Hassan na kueleza kuwa kama kuna mtu ambaye watanzania watamkumbuka basi ni yeye kutokana na hekima na busara zake hasa kwa serikali yake ya awamu ya sita kuwa kiungo kizuri cha kuendeleza yale mazuri yote ya serikali ya awamu yaliyopita

‘’kikubwa anachokifanya kama mama ni hekima, busara na maamuzi yake ni furaha kwa watanzania suala la mariasdhiano lililofanyika ninachotaka kuwaomba wana ccm wenzangu maridhaino ni mchakato, hoja ya msingi hapa tusizifanya hoja zinazoibuliwa katika mikutano kama hoja za kubishana bali ziwe za kutoa majibu kwa yale yaliyofanyika’’ alisema Dkt Mabula

Mjumbe huyo wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya Chama cha Mapinduzi Taifa alieleza kuwa, wanachotakiwa wana CCM kufanya ni kuisimamia serikali kwa kujibu hoja na kuangalia yale yote yaliyoelekezwa na chama kama yanafanyika kama ilivyopangwa.

Naye Mjumbe wa Halamshauri Kuu ya Taifa Bi. Elen Makungu Bogoje amesema Chama cha Mapinduzi kimeendelea kuisimamia serikali kila mahala na kusisitiza kuwa ipo haja kwa viongozi wa CCM katika kila ngazi kwenda kuisimamia serikali katika miradi yote iliyopo maeneo yao.

‘’Niwaombe viongozi wa CCM katika kila ngazi kwenda kuisimamia serikali ili wapinzani wakose hoja za kusema katika mikutano ya hadhara na kazi hii ya kuisimamia serikali tumeifanya na tunaendelea kuifanya’’. Alisema Ellen

Wajumbe wawili wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa Dkt Angeline Mabula ambaye ni Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi na Ellen Makungu Bogoje waliwasili kwa mara ya kwanza katika mkoa wa Mwanza ambako ndiko wanakotokea tangu wachaguliwe kuwa wajumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM katika Mkutano Mkuu wa Cahama cha Mapinduzi uliofanyika mkoani Dodoma hivi karibuni.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com