Balozi wa Uganda nchini Mhe. Col. Fred Mwesigye akiwa na wajumbe kutoka EWURA, PAU, na EACOP wakiangalia baadhi ya magari makubwa ya mizigo ya (trailers) yanayotengenezwa na Superdoll kwaajili ya mradi wa EACOP
Baadhi ya wajumbe wa menejimenti ya EWURA, PAU, EACOP na Superdoll wakimsikiliza Balozi wa Uganda nchini Tanzania, Mhe. Fred Mwesigye(hayupo pichani) mara baada ya kikao cha siku moja kuhusu mradi wa bomba la mafuta ghafi wa EACOP kilichofanyika katika ofisi za Superdoll, leo Januari 29,2023 jijini Dar es Salaam.
Balozi wa Uganda nchini Tanzania, Mhe. Fred Mwesigye (aliyekaa katikati) akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wajumbe wa menejimenti ya EWURA, PAU, EACOP na Superdoll mara baada ya kikao cha siku moja kuhusu mradi wa bomba la mafuta ghafi wa EACOP kilichofanyika katika ofisi za Superdoll, leo Januari 29,2023 jijini Dar es Salaam.
........................
Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA) na Mamlaka ya Petroli Uganda (PAU), leo tar 29/01/2023 imeanza ukaguzi wa maendeleo ya ujenzi 0wa bomba la mafuta ghafi (EACOP) litakaloanzia Hoima Uganda hadi katika bandari ya Tanga.
Ukaguzi huo umeanza kwa kikao kazi cha siku moja, katika kampuni ya Superdoll jijini Dar es Salaam, ambayo imepewa mkataba wa kutengeneza matela(trailers) makubwa yenye uwezo wa kubeba mizigo isiyo ya kawaida, yenye urefu wa mita 21.7 ambapo kati ya hizo mita 18 kwa ajili ya kubeba mabomba makubwa.
Kikao hicho kimehudhuriwa na Balozi wa Uganda nchini Tanzania, Mhe. Col. Fred Mwesigye, Wajumbe wa Bodi ya PAU pamoja na Menejimenti ya PAU na EWURA.
Aidha, Mhe. Mwesigye amepongeza ushirikishwaji wa kampuni za wazawa katika kutekeleza mradi huo, ambapo Superdoll ni kampuni inayomilikiwa na Watanzania 100%, na hadi sasa imeshatengeneza magari 120 kwa ajili ya mradi huo.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Super, Bw. Fulgence Bube, ameishukuru EWURA kwa kuweka utaratibu mzuri na rahisi wa kusajili watoa huduma wazawa katika kanzidata ya EWURA, ili kuwawezesha kutoa huduma katika miradi ya gesi na mafuta hapa nchini ambazo hapo awali zilikua zinachukuliwa na kampuni za kigeni.
Kwa mujibu wa Sheria ya Petroli ya Mwaka 2015, EWURA ina wajibu wa kutoa kibali cha ujenzi wa bomba hilo, pia kuhakikisha shughuli zote za ujenzi zinafanyika kwa kuzingatia viwango vinavyokubalika kimataifa (Petroleum Industry Standards).
Social Plugin