Jeshi la Polisi mkoa wa Mbeya, linamshikilia Joyce Matingo (26), mkazi wa Unyamwanga wilaya ya Rungwe, mkoani Mbeya kwa tuhuma za kumuua mtoto wake aitwaye Emily Matingo(9) kwa kumpiga sehemu mbalimbali za mwili wake.
Kamanda wa Polisi mkoa wa Mbeya, Kamishna Msaidizi wa Jeshi la Polisi ACP Benjamin Kuzaga, amesema kuwa tukio hilo limetokea Januari 8 mwaka huu majira ya saa 12:00 jioni.
Kamanda Kuzaga ametoa wito kwa wazazi na walezi kuacha tabia ya kujichukulia sheria mkononi ikiwa ni pamoja na kutoa adhabu zilizopitiliza na kusababisha madhara makubwa ikiwemo na kutoa uhai wa wengine.
Via: EATV
Social Plugin