Na Abel Paul wa Jeshi la Polisi
Wananchi katika Mkoa wa Arusha wamehimizwa kushiriki na kuweka mazingira safi katika kudhibiti Magonjwa ya milipuko katika Mkoa huo.
Hayo yamesemwa leo Januari 13, 2023 na Mkuu wa Polisi wilaya ya Arusha na Mrakibu mwandamizi wa Polisi SSP GEORGE MALEMA wakati Jeshi la Polisi likifanya usafi katika soko la kilombero lililopo halmashauri ya Jiji la Arusha ambapo amesema dhamira ya Jeshi hilo ni kuhimiza usafi ili kuepuka magojwa ya milipuko.
Malema amesema kuwa Jeshi hilo linadhamana ya kuwalinda wananchi pamoja na mali zao ambapo amebainisha kuwa wao wanaona fahari kuwahudumia wananchi wanaoishi mazingira safi na salama.
Sambamba na hilo amesema Jeshi hilo lina mkakakati wa dhati wa kupunguza na kumaliza kabisa uhalifu ambapo amesema wamekuja na utaratibu huo wa kushirikisha jamii katika kuibua na kupambana na uhalifu.
Kwa Upande wake James Lobikoki Mkuu wa kitengo cha kudhibiti wa taka na usafi wa mji amelishukuru Jeshi la Polisi Mkoa wa Arusha kwa namna walivyo shirikiana na wananchi kufanya usafi katika soko la Kilombero.
Nao badhi ya wafanya biashara wa soko hilo wameliomba Jeshi la Polisi kuendelea kushirikiana na wananchi katika maswala ya kijamii hususani la kufanya usafi na isiwe ndio mwisho.
Naye mkaguzi Msaidizi wa Polisi A/INSP GLORY CHAO ambaye ni mkaguzi wa kata Levolosi amebainisha kuwa wamefanya usafi kupitia mkakati wa Polisi wa kuwashirikisha wananchi katika Mapambano dhidi ya uhalifu katika Jamii.
Social Plugin