Mwenyekiti wa Taasisi ya Desk & Chair Foundation Alhaj Muhamad Sibtain ametunukiwa shahada ya heshima ya uzamili (PhD) toka chuo Kikuu cha American University.
Bwana Sibtain ametunukiwa PhD ya heshima kutokana na kamati ya amani ya Dunia kutambua mchango wake kwa jamii wa kutoa huduma bila ubaguzi na huduma nyingi anazozitoa kuwa ni huduma za kijamii.
Chuo hicho chenye tawi Tanzania kiliwatunuku watu sita kuwa madaktari wa heshima kutokana na michango yao kwa jamii.
Bwana Doktari Sibtain amekuwa mstari wa mbele kwenye kutoa huduma za kijamii Nchini Tanzania bila ubaguzi.
Pia amekuwa mstari wa mbele kwenye kufanya kazi na vyombo vya habari pamoja na kusaidia program mbalimbali za kuwaendeleza waandishi wa habari.
Kwa upande wake Doktari Sibtain amewashukuru watanzania wote kwa kumuunga mkono kwenye utekelezaji wa huduma za kijamii anazozifanya.
"Nimefarijika sana kwa kutunukiwa udaktari wa heshima, naishukuru familia yangu ndugu jamaa na marafiki wote" alisema Sibtain.