NA EMMANUEL MBATILO, DAR ES SALAAM
BARAZA la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC) wamesaini mkataba wa miaka mitatu wa ushirikiano na Taasisi inayojishughulisha na masuala ya kisayansi na kimazingira kutoka nchini India ambapo ushirikiano huo utasaidia kufanya maboresho katika ukusanyaji wa taka ngumu.
Akizungumza na waandishi wa habari leo Januari 23,2023 Jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi wa Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC) Dkt. Samuel Gwamaka amesema NEMC pamoja na Center for Science and Environment wamekusudia kujengeana uwezo na uzoefu kuwa pamoja na kufanya tafiti zinazohusiana na miji yetu katika ukusanyaji taka lakini vilevilekubadilishana uzoefu ambapo baadhi ya wataalamu wao wanaweza kupewa mafunzo.
Amesema nia ya mkataba huo uwe wa miaka mitatu kuanzia sasa lakini kutakuwa na uwezekano kuupeleka mbele zaidi lengo kubwa ni kuzipa nguvu Mamlaka za Serikali za Mitaa hasa katika majiji, miji pamoja na Wilaya ndo maana wakurugenzi wameweza kushiriki kwenye mkutano huo ili waweze kubadilishana mawazo na uzoefu ili baadae tuwe na mifumo ya kisasa kuhakikisha taka ngumu zinazozalishwa ziwezwe kutengwa na zisionekane kwenye madampona zile zinazooza ziweze kuwa mbolea.
"Suala la taka ngumu limekuwa changamoto katika miji mingi sio Tanzania tu,lakini katikanchi mbalimbali kwahiyo tumekuwa na wenzetu kutoka nchi mbalimbali ikiwemo Rwanda, Kenya, Uganda, Ethiopia, Eswatini, Ghana , Zambia ambao na wao wametuma wawakilishai wao hapa kuja kujadili na kuweza kubadilishana uzoefu". Amesema
Aidha amesema madampo imekuwa mojawapo ya sehemu ambayo ni changamoto na ni gharama katika kuyaendesha katika uksanyaji wa taka ngumu na matokeo yake miji yetu mingi imekuwa ni michafu hivyo kupitia Taasisi hiyo kutoka India ambao wao wamekwenda mbali katika teknolojia hivyo kusaidia kutengeneza mifumo rafiki kwaajili ya kutenga taka ngumu zisiweze kuleta madhara kwenye mazingira.
Kwa upande wake Mwakilishi kutoka OR TAMISEMI, Bi.Hawa Mwechaga amesema TAMISEMI inasimamia halmashauri 184 ambako huko kote kuna taka ngumu kwahiyo kwa kila halmashauri wana idara zinazoratibu uzalishaji wa taka ngumu hivyo wanashirikiana na NEMC kuona ni namna gani wanaenda kuboresha Majiji na miundombinu mbalimbali.
Social Plugin