Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum, Wakili Amon Mpanju,akizungumza wakati akifungua kikao kazi cha Wakuu wa Vyuo vinavyotoa mafunzo ya Malezi wa Watoto nchini kilichofanyika leo Januari 19,2023 jijini Dodoma.
Sehemu ya washiriki wakimsikiliza Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum, Wakili Amon Mpanju,wakati akifungua kikao kazi cha Wakuu wa Vyuo vinavyotoa mafunzo ya Malezi wa Watoto nchini kilichofanyika leo Januari 19,2023 jijini Dodoma.
Kamishna wa Ustawi wa Jamii kutoka Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum,Dkt. Nandera Mhando,akizungumza wakati wa kikao kazi cha Wakuu wa Vyuo vinavyotoa mafunzo ya Malezi wa Watoto nchini kilichofanyika leo Januari 19,2023 jijini Dodoma.
Mkurugenzi Msaidizi anayesimamia huduma za Jamii Ofisi ya Raisi-TAMISEMI Bi Amina Mfaki,akizungumza wakati wa kikao kazi cha Wakuu wa Vyuo vinavyotoa mafunzo ya Malezi wa Watoto nchini kilichofanyika leo Januari 19,2023 jijini Dodoma.
Kaimu Mkurugenzi Idara ya watoto kutoka Wizara ya Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wanawake na Makundi Maalum Bi Asha Shami,akizungumza wakati wa kikao kazi cha Wakuu wa Vyuo vinavyotoa mafunzo ya Malezi wa Watoto nchini kilichofanyika leo Januari 19,2023 jijini Dodoma.
Mkurungenzi wa Shirika lisilo la kiserikali la Karibu Tanzania Organization (KTO) Bw.Majid Mjengwa,akielezea taasisi hiyo ilivyoanza mpango huo wakati wa kikao kazi cha Wakuu wa Vyuo vinavyotoa mafunzo ya Malezi wa Watoto nchini kilichofanyika leo Januari 19,2023 jijini Dodoma.
Mkuu wa Chuo cha Maendeleo ya Wananachi Karumo Bi.Osmunda Kilasi,akizungumzia umuhimu wa mpango huo wakati wa kikao kazi cha Wakuu wa Vyuo vinavyotoa mafunzo ya Malezi wa Watoto nchini kilichofanyika leo Januari 19,2023 jijini Dodoma
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum, Wakili Amon Mpanju,akiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kufungua kikao kazi cha Wakuu wa Vyuo vinavyotoa mafunzo ya Malezi wa Watoto nchini kilichofanyika leo Januari 19,2023 jijini Dodoma.
.......................................
Na Alex Sonna-DODOMA
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum, Wakili Amon Mpanju amewataka watoa Mafunzo ya Walezi wa Watoto nchini kuwa na Mpango kazi wa pamoja utakaotumika kuwafundishia walezi wa Watoto.
Hayo ameyasema leo Januari 19,2023 jijini Dodoma wakati akifungua kikao kazi cha Wakuu wa Vyuo vinavyotoa mafunzo hayo ya Malezi.
“Kuna haja ya kuja na Mtaala wa pamoja ili kutatua changamoto ya Malezi na Makuzi ya Awali kwa watoto. Iwepo pia bodi ya usimamazi na Mwongozo utakaosaidia kuratibu eneo hili ili wahitimu wawe na Ujuzi utakaosaidia Watoto wetu”Alisema Wakili Mpanju.
Wakili Mpanju amewasisitiza Wadau hao juu ya umuhimu wa kuwekeza kwenye malezi na makuzi ya awali ya Watoto Nchini Ili kujenga watu wenye maadili na nidhamu kwa Taifa.
Mpango wa ufundishaji wa mtaala mmoja uliasisiwa na Shirika lisilo la kiserikali la Karibu Tanzania Organization (KTO) ambao walianza mafunzo kwa chuo kimoja Kisha wakapeleka kwa vyuo 10 kati ya 54 vya Maendeleo ya Jamii.
“Tusipowekeza vya kutosha tutapata majanga ,Mnyonyoko wa Maadili utaendelea na hatimaye Taifa litapotea.”Ameongeza Mpanju.
Kwa upande wake Kamishna wa Ustawi wa Jamii,Dkt. Nandera Mhando amesema lengo ni kuweza kufikia yale yaliyokusudiwa kupatikana kwenye Vyuo hivyo vinavyotoa Mafunzo kwa walezi Wa Watoto.
“Kwa pamoja tuweke igezo vya pamoja ikiwemo Mitaala na mitihani ili tuweze kupata Wahitimu wanaokidhi na hatimaye kufanikisha nia ya Serikali kupitia Wizara ya Maendeleo ya Jamii”amesema Dk.Mhando
Aidha Dk.Mhando amesema kuwa msingi uliopandwa na KTO unapaswa kuendelezwa ili kuzaa matunda yatakayosambaa nchi nzima badala ya kuwa walalamikaji kuhusu kuharibiwa kwa maadili ya watoto.
Naye Mkurungenzi wa Shirika lisilo la kiserikali la Karibu Tanzania Organization (KTO) Bw.Majid Mjengwa amesema kuwa taasisi hiyo ilianza mpango huo mapema kwa kushirikiana na baadhi ya vyuo ndipo wakabaini kwamba kuna ulazima wa kupeleka elimu hiyo Kwa vyuo vyote.
Mjengwa amesema mwelekeo wa sasa ni kuona mtoto wa Kitanzania analelewa na kufundishwa misingi impasayo mwanadamu kuliko ilivyo sasa ambapo vituo ni vingi lakini kila mmoja anatoa mafunzo ya mwelekeo wake.
Hata hivyo Bw. Mjengwa amesema kuwa mitaala inayotazamwa ni ya vituo vya watoto wadogo (Day care) ambako ndiko uliko msingi wa Mkuu wa ujifunzaji kwa mwanafunzi.
"Tunashukuru Serikali imekubali mpango huu na kuahidi kupeleka vyuo vyote 54, hili ni jambo jema sana kwamba tunakwenda kuzalisha wataalamu wazuri wa malezi ya watoto Wetu," amesema Bw. Mjengwa.
Mkurugenzi Msaidizi anayesimamia huduma za Jamii Ofisi ya Raisi-TAMISEMI Bi Amina Mfaki amesema Serikali inatoa kipaumbele kwa malezi na Makuzi ya Awali kwa watoto Nchini ili kujenga Taifa la Wananchi Wazalendo.
“Mnaowandaa Walezi wa Watoto mna jukumu kubwa la kuhakikisha Mafunzo yanayotolewa Vyuoni yanaweza kuwakuza watoto na Vipaji vyao na Mwisho wa siku tutapata vijana wabunifu watakaoleta Maendeleo katika Taifa letu”amesema Bi.Mfaki
Awali Kaimu Mkurugenzi Idara ya watoto kutoka Wizara ya Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wanawake na Makundi Maalum Bi Asha Shami amesisitiza juu ya Maudhui ya kuzingatia katika utoaji wa Elimu ya Awali kwa Watoto.
“Tunategemea mtawalinda watoto kwa kuzingatia maudhui sahihi katika ufundishaji maana kumekua na changamoto nyingi za kimaadili zitokanazo na vitu ambavyo watoto wanajifunza mashuleni na Majumbani,Hivyo Maudhui yenye kuzingatia Mila na Tamaduni zetu ni muhimu.”Alisema Bi Asha .
Nao Wakuu wa Vyuo na Wadau wanaotoa Mafunzo Kwa Walezi wa Watoto Nchini wameiomba Serikali kuhakikisha Mchakato wa kupata Mtaala wa Pamoja Nchini unakamilika Haraka ili waweze kuuanza kuutumia Katika Mafunzo yao .
Social Plugin