******************
NA EMMANUEL MBATILO, DAR ES SALAAM
KLABU ya Simba imefanikiwa kuichapa Mbeya City kwa mabao 3-2, mchezo ambao ulipigwa kwenye dimba la Bejamini Mkapa Jijini Dar es Salaam.
Simba Sc ilianza kupata bao la kwanza kupitia kwa Saidi Ntibazonkiza dakika 11, aliefunga bao zuri na kuhamsha shangwe za mashabiki waliongia kwenye uwanja huo kushuhudia mchezo huo ambao ulikuwa wa aina yake.
Ntibazonkiza ameendelea kuuwasha moto ndani ya uzi wa msimbazi baada ya kufanikiwa kupachika bao la pili dakika 49 ambalo likafanya afikishe mabao tisa kwenye ligi hiyo.
Bao la tatu Simba Sc limefungwa na Pape Sakho dakika ya 56 ya mchezo, huku mabao ya Mbeya City yakifungwa na Richardson Ng'ondya dakika ya 13 na bao la pili likifungwa na Juma Shemvuni dakika ya 78 na mechi kuisha Simba Sc kuondoka na ushindi wa mabao 3-2.
Social Plugin