WAZIRI AWASILISHA AZIMIO LA MKUTANO MKUU WA ILO KATIKA KAMATI YA BUNGE


Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu), Prof. Joyce Ndalichako, akiwasilisha azimio la kujumuisha suala la Usalama na Afya Mahali pa Kazi katika misingi minne ya awali ya Shirika la Kazi Duniani (ILO) ya haki katika maeneo ya kazi katika vikao vya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Katiba na Sheria vinavyoendelea jijini Dodoma. 


Mtendaji Mkuu wa OSHA, Khadija Mwenda, akijibu baadhi ya hoja za wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Katiba na Sheria katika kikao cha Kamati hiyo ambacho Waziri Mwenye Dhamana ya Masuala ya Kazi, Prof. Ndalichako, aliwasilisha azimio la ILO ambalo suala la Usalama na Afya Mahali pa Kazi lilijumuishwa katika misingi minne ya awali ya Shirika hilo ya haki katika maeneo ya kazi. 

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu), Prof. Joyce Ndalichako (wakwanza kushoto) pamoja na wajumbe Kamati ya Bunge ya Katiba na Sheria wakifuatilia mada ya mafunzo ya huduma ya kwanza yaliyotolewa na OSHA kwa wajumbe wa Kamati hiyo. 

Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Katiba na Sheria, Joseph Mhagama (kushoto) akifuatilia wasilisho la Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu), Prof. Joyce Ndalichako, katika kikao cha Kamati hiyo. 


Mtendaji Mkuu wa OSHA, Khadija Mwenda (mwenye suti nyeusi), akiwa na baadhi ya watendaji katika Ofisi yake wakifuatilia wasilisho la Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu), Prof. Joyce Ndalichako, kuhusu azimio lililopitishwa na Nchi Wanachama wa Shirika la Kazi Duniani katika Mkutano wa 110 uliofanyika Geneva Uswisi Juni mwaka jana. 


Baadhi ya wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Katiba na Sheria wakifuatilia wasilisho la Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu), Prof. Joyce Ndalichako, kuhusu azimio lililopitishwa na Nchi Wanachama wa Shirika la Kazi Duniani katika Mkutano wa 110 uliofanyika Geneva Uswisi Juni mwaka jana. 


Baadhi ya watendaji wa Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) wakiwa katika kikao cha Kamati ya Bunge ya Katiba na Sheria ambacho Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu), Prof. Joyce Ndalichako, aliwasilisha azimio lililopitishwa na Nchi Wanachama wa Shirika la Kazi Duniani katika Mkutano wa 110 uliofanyika Geneva Uswisi Juni mwaka jana.

Mkufunzi wa OSHA, Moteswa Meda, akiwasilisha mada kuhusu masuala ya huduma ya kwanza mahali pa kazi katika Kamati ya Bunge Katiba na Sheria ambapo wajumbe wa Kamati hiyo wamefundishwa kwa vitendo namna ya kuwahudumia wafanyakazi wanaopata changamoto mbali mbali za kiafya mahali pa kazi ikiwemo kupoteza fahamu, kuumia, kupata athari za sumu na kemikali. 

*********** 

Na Mwandishi Wetu 

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu), Prof. Joyce Ndalichako, amewasilisha azimio la kujumuisha suala la Usalama naAfya Mahali pa Kazi katika misingi minne ya awali yaShirika la Kazi Duniani (ILO) ya haki katika maeneo yakazi katika vikao vya Kamati ya Kudumu ya Bunge yaKatiba na Sheria vinavyoendelea jijini Dodoma. 

Azimio hilo lilipitishwa na kwa kauli moja na NchiWanachama wa ILO (Tanzania ikiwemo) katika MkutanoMkuu wa 110 wa Shirika la Kazi Duniani uliofanyikaGeneva, Uswisi kuanzia tarehe 27 Mei hadi tarehe 11 Juni, 2022 ambapo Waziri Mwenye Dhamana yaMasuala ya Kazi, Prof. Ndalichako alihudhuria akiwaameambatana na Mtendaji Mkuu wa Wakala waUsalama na Afya Mahali pa Kazi (OSHA), Khadija Mwenda pamoja na watendaji wengine wa Ofisi yaWaziri Mkuu (Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu). 

Misingi ya awali ya ILO ya haki mahali pa kazi ni pamojana; Uhuru wa kujumuika na utambuzi wa haki yamajadiliano ya pamoja (freedom of association and the effective recognition of the right to collective bargaining),Kukomesha mifumo yote ya kazi za kushurutishwa nakulazimishwa (the elimination of all forms of forced or compulsory labour), Kukomesha ajira za watoto (the effective abolition of child labour), na Kukomesha kwaubaguzi kwenye ajira na mahali pa kazi (the elimination of discrimination in respect of employment and occupation). 

Kwa mujibu wa azimio hilo lililopitishwa mwaka jana, suala la usalama na afya mahali pa kazi (a safe and healthy working environment) unakuwa ni msingi watano wa haki katika maeneo ya kazi. 

Akiwasilisha azimio hilo mbele ya Kamati ya Katiba naSheria, Waziri Ndalichako, amesema, Ofisi ya Waziri Mkuu imeona ni muhimu kuishirikisha Kamati kuhusuazimio hilo ili kuiwezesha kuyafahamu mabadiliko hayona hivyo kuendelea kutekeleza jukumu lake la kuishauriOfisi ya Waziri Mkuu na Taasisi ya OSHA ipasavyohususan katika masuala Usalama na Afya nchini. 

“Waheshimiwa wabunge tumeona ni vema tukawasilishakwenu azimio hili ambalo limepitishwa na NchiWanachama wa Shirika la Kazi Duniani na nchi yetuikiwemo hivyo kutokana na azimio hili masuala yaUsalama na Afya mahala pa kazi yanakuwa si wajibuwa Kisheria pekee bali haki ya msingi mahali pa kazi,” Waziri Ndalichako ameieleza Kamati ya Katiba naSheria. 

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu yaBunge ya Katiba na Sheria, Joseph Mhagama, amemshukuru Waziri Ndalichako kwa jitihadaanazofanya katika kuhakikisha kwamba Kamati hiyoinawezeshwa kutekeleza jukumu lake la kuisimamiaOfisi ya Waziri Mkuu na Taasisi chini yake kupitiasemina na mafunzo mbali mbali ambayo amekuwaakiyaandaa kupitia Taasisi anazoziongoza. 

Nae Mtendaji Mkuu wa OSHA, Khadija Mwenda,ameishukuru Kamati kwa miongozo na ushauri ambaoimekuwa ikiitoa katika kuendelea kuboresha masuala yaUsalama na Afya mahali pa kazi ambapo ameahidiTaasisi yake kuendelea kufanya kazi kwa bidii pamojana kutekeleza maelekezo na kufanyia kazi ushauriambao umekuwa ukitolewa na Kamati hiyo. 

Wasilisho hilo la Waziri Ndalichako katika Kamati, limefanyika sambamba na mafunzo ya huduma yakwanza mahali pa kazi ambapo wabunge hao wamefundishwa kwa vitendo namna ya kuwahudumiawafanyakazi wanaopata changamoto mbali mbali za kiafya mahali pa kazi ikiwemo kupoteza fahamu, kuumia, kupata athari za sumu na kemikali. 

OSHA ni Taasisi ya Serikali chini ya Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) wenyejukumu la kusimamia utekelezaji wa Sheria ya Afya naUsalama Mahali pa Kazi ya mwaka 2003. Sheria hiipamoja na mambo mengine inawataka waajiri wotekuhakikisha kwamba maeneo yao ya kaziyanatambulika na OSHA ili kufikishiwa huduma muhimuukiwemo ukaguzi wa usalama na afya, ushauri wakitaalam pamoja mafunzo muhimu ya usalama na afyamahali pa kazi.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com
Previous Post Next Post