Mratibu wa Elimu ya Afya kwa Umma Mkoa wa Shinyanga, Mwita Thomas akitoa elimu kuhusu UVIKO - 19 kwa waandishi wa habari Mkoa wa Shinyanga.
Na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Ofisi ya Mganga Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga kwa kushirikiana na Shirika lisilo la Kiserikali la Afya Plus imetoa mafunzo kwa Waandishi wa Habari katika Wilaya ya Shinyanga na Kishapu kuhusu UVIKO-19 huku hamasa ikiwa ni vyombo vya habari kuendelea kuhamasisha wananchi kuchukua tahadhari dhidi ya UVIKO-19 ikiwemo kupata chanjo.
Mafunzo hayo yamefanyika leo Ijumaa Februari 10,2023 katika ukumbi wa Hospitali ya Mkoa wa Shinyanga yakishirikisha waandishi wa habari wanaoandikia vyombo vya habari na Maafisa Habari wa Halmashauri wa wilaya ya Kishapu na Manispaa ya Shinyanga.
Akizungumza wakati wa mafunzo hayo, Mratibu wa Elimu ya Afya kwa Umma Mkoa wa Shinyanga, Mwita Thomas amesema licha ya kwamba mkoa huo umefikia asilimia 100 ya utoaji wa chanjo ya UVIKO – 19, vyombo vya habari vina wajibu wa kuendelea kuhamasisha wananchi kuchukua tahadhari dhidi ya UVIKO – 19 kwa kunawa mikono mara kwa mara na kupata chanjo ya UVIKO – 19.
“Mkoa wa Shinyanga una chanjo za UVIKO- 19 za kutosha na zinatolewa bure, chanjo hizi ni salama hakuna madhara yoyote ya chanjo. Lengo la mkoa huu ni kuongeza zaidi kiwango cha uchanjaji kwani bado kuna makundi ya vijana na wazee hayajafikiwa”,ameeleza Thomas.
“Hospitali zetu pia zinaendelea kutoa huduma ya kupima UVIKO – 19. Naomba wananchi waendelee kupata chanjo ya UVIKO – 19. Tunaendelea kutekeleza afua za UVIKO-19 kwa kushirikiana na wadau mbalimbali wakiwemo Afya Plus ambao wanatekeleza mradi katika wilaya ya Kishapu na Shinyanga”,amesema Thomas.
Kwa upande wake, Afisa Ufuatiliaji wa shirika la Afya Plus, Silvana Chimombo amesema wanaendelea kushirikiana na serikali katika mapambano dhidi ya UVIKO-19 hivyo kuwaomba wananchi kuendelea kupata chanjo dhidi ya ugonjwa huo.
Nao waandishi wa habari wameahidi kutumia kalamu zao kuhamasisha jamii kuendelea kupata chanjo ya UVIKO – 19 pamoja kuchukua tahadhari dhidi ya ugonjwa huo.
Mratibu wa Elimu ya Afya kwa Umma Mkoa wa Shinyanga, Mwita Thomas akitoa elimu kuhusu UVIKO - 19 kwa waandishi wa habari Mkoa wa Shinyanga. Picha na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Mratibu wa Elimu ya Afya kwa Umma Mkoa wa Shinyanga, Mwita Thomas akitoa elimu kuhusu UVIKO - 19 kwa waandishi wa habari Mkoa wa Shinyanga.
Mratibu wa Elimu ya Afya kwa Umma Mkoa wa Shinyanga, Mwita Thomas akitoa elimu kuhusu UVIKO - 19 kwa waandishi wa habari Mkoa wa Shinyanga.
Afisa Ufuatiliaji wa shirika la Afya Plus, Silvana Chimombo akitoa elimu kuhusu UVIKO - 19 kwa waandishi wa habari Mkoa wa Shinyanga.
Afisa Ufuatiliaji wa shirika la Afya Plus, Silvana Chimombo akitoa elimu kuhusu UVIKO - 19 kwa waandishi wa habari Mkoa wa Shinyanga.
Waandishi wa habari Mkoa wa Shinyanga wakiwa ukumbini
Waandishi wa habari Mkoa wa Shinyanga wakiwa ukumbini
Waandishi wa habari Mkoa wa Shinyanga wakiwa ukumbini
Waandishi wa habari Mkoa wa Shinyanga wakiwa ukumbini
Mafunzo yanaendelea
Waandishi wa habari Mkoa wa Shinyanga wakiwa ukumbini
Mafunzo yanaendelea
Waandishi wa habari Mkoa wa Shinyanga wakiwa ukumbini
Social Plugin