Polisi katika kaunti ya Bungoma nchini Kenya wanachunguza kisa ambapo mwanamke anadaiwa kumng'ata baba mkwe wake sehemu za siri wakati wa ugomvi.
Katika kisa hicho cha kustaajabisha ambacho kimeshtua familia na majirani, Vincent Simiyu mwenye umri wa miaka 78, kutoka kijiji cha Kimaeti eneobunge la Bumula, anauguza majeraha kufuatia kuumwa uume wake na mkaza mwana wake.
Kulingana na mashahidi, mshukiwa Everline Okelo, anadaiwa kukasirishwa na baba mkwe wake baada ya kupata fununu kwamba alikuwa anafahamu mwanawe alioa mke wa pili. Simiyu alisimulia kuwa Okelo alimpiga kwa jiwe na kuanguka chini na baadaye kumkalia kifuani huku akimshika uume wake alioweka mdomoni na kuuma.
"Alichukua mawe, akanipiga kwa mgongo nikaanguka chini nikakosa fahamu, bibi ya mtoto yangu akaniangukia anakikalia kwa kifua, akaniuma, nikamskuma, akanishika kwa long'i, akakunja sehemu nyeti akaweka kwa mdomo yake, akaniuma, nikalia ndio mtoto wangu akakuja kuniokoa," alisimulia babu.
Zogo hilo lilivutia majirani ambao walimpa kichapo mwanamke huyo na mumewe na kumkimbiza mzee huyo hospitalini.
Kisha baadaye mwanamke huyo aliingia mafichoni na sasa nado anasakwa. Wazee wa Bukusu walisema mwanamke huyo ni lazima aadhibiwe kitamaduni kwa kuwa mila za jamii hiyo zinamzuia kukaribiana kimwili na wakwe zake. Kanuni, maadili na imani za ajabu ya ndoa ya Bukusu Jila jamii kote duniani ina maadili na imani zake, na hii inatimiza heshima katika kiwango fulani. Iwapo unatarajia kuolewa na jamaa kutoka katika jamii ya Bukusu, ni vyema kujifunza kuhusu kanuni kadhaa zinazoweza kusaidia maisha yako ya ndoa.
Bukusu ni kabila dogo la jamii ya Waluhya, ambalo ni mojawapo ya makabila makubwa zaidi katika Afrika Mashariki na Kati. Jamii hiyo inapatikana zaidi katika kaunti za Bungoma na Trans Nzoia. Jumuiya inajivunia desturi za kipekee za kitamaduni za kiasili ambazo zitakuacha uvutiwe. Moja ya tamaduni hizo ni kwamba baada ya kuingia katika nyumba wakwe, usifunge milango yoyote. Kimsingi mtu haruhusiwi kuwa katika nyumba moja na mama mkwe au baba mkwe wake na milango imefungwa hivyo milango yote yanatakiwa kuwa wazi wakati wanapokutembelea au unapowatembelea.