Mwanaume mmoja raia wa Marekani ambaye alikaa gerezani kwa takriban miaka 28 kwa kosa la mauaji ambayo amekuwa akiyakanusha kufanya ameachiwa huru huko Missouri.
Lamar Johnson, mwenye umri wa miaka 50, alitoka nje ya chumba cha mahakama ya St Louis mtu huru baada ya uamuzi wa Jaji David Mason siku ya Jumanne.
Jaji alisema alichukua hatua baada ya mashahidi wawili kutoa "ushahidi wa wazi na wa kushawishi" kwamba Bw Johnson hana hatia.Alipatikana na hatia ya kumuua Marcus Boyd mwaka 1994.
Bw Johnson alionekana kuguswa wakati uamuzi huo ulipotangazwa, huku wafuasi wake wakianza kushangilia na kupongeza.
Baada ya kuachiwa .Bw Johnson alisema tukio hilo ni la aina yake kwenye maisha yake baada ya kuondoka katika chumba cha mahakama.
Mwaka jana, Wakili Kim Gardner alikuwa amewasilisha hoja ya kutaka kuachiliwa kwa Bw Johnson baada ya kufanya uchunguzi pamoja na shirika la kisheria lisilo la faida la Innocence Project.
Social Plugin